Bodi ya Nishati Vijijini Yapongeza Uzalishaji wa Vifaa vya Miradi ya Umeme

Tuesday, July 30, 2019|Number of views (2911)|Categories: News, Announcements
Bodi ya Nishati Vijijini Yapongeza Uzalishaji wa Vifaa vya Miradi ya Umeme
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo amevipongeza viwanda vinavyotengeneza vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwa uzalishaji wa vifaa kwa kiwango kikubwa unaochochea ukuaji wa sekta ya nishati nchini.

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ilifanya ziara ya kutembelea viwanda vinavyotengeneza vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Njombe na Iringa ili kujionea shughuli za uzalishaji vifaa hivyo.
Katika ziara hiyo, wamiliki wa viwanda vya vifaa vya umeme wameahidi kuendelea kuzalisha vifaa hivyo kwa kiwango kikubwa ili kukidhi mahitaji ya miradi ya umeme nchini.

Wakili Kalolo alisema ameridhishwa na kasi ya uzalishaji wa vifaa katika viwanda hivyo na kusisitiza umuhimu wake katika kufanikisha kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya nishati vijijni ambayo inaendelea nchini, ambapo mpaka sasa ni vijiji 7400 kati ya 12,268 vimeunganishwa na huduma ya umeme.
“Ziara hii imetusaidia kujua changamoto wanazokumbana nazo wazalishaji wa vifaa vya umeme, lakini pia naweza kuthibitisha uwezo wao baada ya kutembelea viwanda hivi, ni wazi kwamba suala la nguzo za umeme tunajitosheleza kwa viwanda vyetu, suala la mita na waya sio changamoto, vyote vinazalishwa ndani ya nchi”, aliongeza Wakili Kalolo.

Pia Wakili Kalolo amewapongeza wamiliki wa viwanda hivyo kwa kuajiri wafanyakazi wazawa kwa wingi na kuwataka kuendelea kuongeza wafanyakazi wanaopatikana hapa hapa nchini Tanzania. Wakili Kalolo aliongeza kusema kuwa, Serikali imetengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuhakikisha kuwa juhudi za Rais John Magufuli kwamba Serikali itafikia uchumi wa kati kufikia Mwaka 2025.

Akielezea umuhimu wa viwanda hivyo katika utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga amesema watengenezaji wa vifaa vinavyotumika katika miradi ya umeme, kama vile mita, waya, transfoma, nguzo na vingine vingi ni wadau muhimu sana katika kuleta mabadiliko chanya ya maendeleo vijijini kupitia nishati ya umeme.

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania

Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

«August 2020»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
2178

MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI ATOA WITO KUHUSU ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.
Read more
10
2179

REA YAIBUKA NA USHINDI MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2020 MKOANI SIMIYU

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Read more
111213141516
17181920212223
24252627282930
31123456