Mradi Mpya wa Kusambaza Umeme Pembezoni mwa Miji na Majiji Wazinduliwa

Saturday, August 10, 2019|Number of views (4000)|Categories: News, Announcements
Mradi Mpya wa Kusambaza Umeme Pembezoni mwa Miji na Majiji Wazinduliwa
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye vijiji na mitaa viliyopo pembezoni mwa miji na majiji. Katika nyakati na maeneo tofauti, uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Nishati Mh. Dk Medard Kalemani (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu (Mb) katika maeneo ya Kigamboni, Kisarawe, Mkuranga, Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo na Chalinze.

Akizindua Mradi huo ambao unajulikana kama Peri-urban electrification katika Wilaya ya Kigamboni, Waziri wa Nishati Mh. Dk Medard Kalemani (Mb) alisema Serikali ya Awamu ya Tano iliamua kuanzisha mradi huu ili kuwasambazia umeme wananchi ambao vijiji au mitaa yao kijiografia inaonekana ipo mijini lakini haijafikiwa na miundombinu kusamba umeme.
Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu (Mb) ameagiza kifaa cha UMEME TAYARI (UMETA) kifungwe katika nyumba za wananchi ambao ni walemavu, wajane na wenye kipato cha chini ili nao waweze kunufaika na miradi ya kusambaza umeme vijijini. Mh. Mgalu alitoa agizo hilo wakati akizindua mradi huo katika maeneo ya Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo na Chalinze. Alisema Serikali imetoa UMETA 250 kwa kila LOT ambazo zitatumika kuunganisha umeme kwa wateja ambao ni walemavu, wajane na wenye kipato kidogo.

Mh. Naibu Waziri alisema wateja wengine watanunua kifaa hicho kwa bei ya Shilingi 36,000 tu na kwamba, wale ambao hawatamudu gharama za kutandaza mfumo wa nyaya za umeme katika nyumba zao wakati wa ujenzi wa miundombinu ya miradi.

Akifafanua kuhusu Mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Mhandisi Amos Maganga alisema mradi wa usambazaji nishati ya umeme katika maeneo yaliyo pembezoni mwa miji umeanzishwa kutokana na maombi ya wananchi kupitia wawakilishi wao, ambao waliona nguzo zikipita kwenye miji yao na kupeleka umeme vijijini bila ya wao kunufaika na miundombinu hiyo.

Mhandisi Maganga amesema REA imejipanga kuhakikisha wanavifikia vijiji vyote kwa kufunga transfoma 92 katika maeneo tofauti ya Mkoa wa Pwani ambapo jumla ya shilingi Bilioni 14.9 zitatumika kutekeleza mradi huo.

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania

Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

«August 2020»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
2178

MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI ATOA WITO KUHUSU ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.
Read more
10
2179

REA YAIBUKA NA USHINDI MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2020 MKOANI SIMIYU

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Read more
111213141516
17181920212223
24252627282930
31123456