SUMA JKT WAPONGEZWA KWA KUJENGA MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME

Thursday, August 27, 2020|Number of views (546)|Categories: News, Events
SUMA JKT WAPONGEZWA KWA KUJENGA MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo amekipongeza kikosi cha Suma JKT ambacho kimepewa kazi kujenga miundombinu ya kusambaza umeme katika kata ya Kwa Mtoro na Farkwa na ameonesha nia ya kufanya nao kazi katika miradi mingine inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Wakili Kalolo alitoa pongezi hizo tarehe 25/08/2020 wakati Bodi yake ilipofanya ziara ya siku moja kukagua ujenzi wa Miundombinu ya umeme katika kata ya Farkwa ambapo kikosi kutoka Suma JKT kilikuwa kinaendelea kujenga miundombinu ya kusambaza umeme.

“Ni muda mfupi lakini mmefanya kazi nzuri ambayo inaleta matumaini kwetu tuendelee kushirikiana na kuwe na mawasiliano ya karibu. Kukiwa na jambo lolote gumu msisite kusema ili lipatiwe ufumbuzi haraka. Tunawashukuru na tumeona mnaweza kufanya kazi hizi za miradi ya kusambaza umeme vijijini, hivyo kwenu ni fursa tunapotangaza zabuni na nyie muombe ili muweze kushindanishwa,” alisema Wakili Kalolo.

Aidha, Wakili Kalolo aliwataka Suma JKT waongeze idadi ya watu ili waweze kukamilisha kazi hiyo kwa muda mfupi wananchi waweze kunufaika na umeme.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga alisisitiza kwa kusema “kama Mwenyekiti alivyosema sasa Suma JKT wameingia katika industry ya umeme, pamoja na kuwa hii kazi ni ya dharura tumepata kipimo cha kuweza kuwaona kwamba tunaweza kufanya nao kazi. Tutaendelea kushirikiana nao”.

Naye Kapteni James Mhame, anayesimamia kikosi hicho cha Suma JKT, alisema kuwa wamedhamiria kukamilisha kazi hiyo yenye urefu wa kilomita 14 ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme kwa muda waliopewa.

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz

Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

«October 2020»
MonTueWedThuFriSatSun
2829
2182

Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Sasa ni Kitongoji kwa Kitongoji

Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Merdad Kalemani amezindua Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili tarehe 24 Septemba 2020. Mradi huu unalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji katika vijiji vilivyofikiwa na miundombinu ya umeme.
Read more
301234
5678
2184

Bodi ya Nishati Vijijini Yatembelea Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imefanya ziara ya siku moja katika Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere uliopo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao ukikamilika utawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.
Read more
91011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678