MAFUNZO YA KUENDELEZA TEKNOLOJIA ZA NISHATI JADIDIFU

Tuesday, August 5, 2014|Number of views (8888)|Categories: News, Announcements

Documents to download

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2014/2015 umepanga kutoa mafunzo ya hadi wiki mbili kwa wajasiriamali wanaoendeleza vyanzo vya umeme unaofuliwa kutokana na nishati jadidifu. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo mafundi na waendelezaji wa teknolojia za nishati bora waliopo maeneo ya vijijini ili waweze kutoa huduma bora.

Wakala unakaribisha maombi kutoka kwa mafundi na waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini katika teknolojia zifuatazo:

1. Nishati itokanayo na maporomoko madogo ya maji

2. Nishati itokanayo na tungamotaka (biogas & biomas)

3. Nishati itokanayo na upepo

4. Utayarishaji wa mpango biashara

5. Nishati itokanayo na mionzi ya jua

Sifa za Mwombaji

Waombaji wawe na elimu ya Kidato cha Nne (wenye vyeti vya ufundi VETA Daraja la 1 watapewa kipaumbele)

Maombi yote yatumwe yakiwa na taarifa zifuatazo:

1. Jina, anwani, namba ya simu ya atakayehudhuria mafunzo, kazi anayofanya, uzoefu wake na vivuli v ya vyeti vya elimu aliyonayo.

2. Iwapo maombi yatapitia katika taasisi/mradi wa nishati; Jina kamili la taasisi/mradi wa mwombaji, Jina la atakayehudhuria mafunzo, nakala ya vyeti vya elimu aliyonayo, anwani na namba ya simu ya taasisi ikiwa ni pamoja na maelezo mafupi kuhusu uzalishaji wa chanzo husika, mahali chanzo kilipo, uwezo wake wa kuhudumia jamii au idadi ya wateja wanaotegemea kuunganishwa/kufaidika na huduma hiyo.

Wakala utasimamia na kugharamia mafunzo husika. Mwombaji atatakiwa kugharamia usafiri wa kwenda na kurudi katika mafunzo.

Maombi yatumwe kwenye anuani ifuatayo kabla ya tarehe 15/08/2014.


Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S.L.P. 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Parua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007


Documents to download

«August 2020»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
2178

MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI ATOA WITO KUHUSU ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.
Read more
10
2179

REA YAIBUKA NA USHINDI MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2020 MKOANI SIMIYU

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Read more
111213141516
17181920212223
24252627282930
31123456