TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEKELEZAJI WA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI

Thursday, January 7, 2016|Number of views (3028)|Categories: Press Releases

DAR ES SALAAM, 07 JANUARI 2016

Serikali kupitia Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini (REA/REF) inafadhili miradi ya kusambaza umeme vijijini katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Miradi ya Awamu ya Pili ya Usambazaji Umeme Vijijini inatekelezwa na wakandarasi kutoka sekta binafsi ambao huhusika na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme chini ya usimamizi wa TANESCO.

Malipo ya Huduma kwa Wakandarasi, Wakandarasi Wadogo na Vibarua

Kumekuwepo na malalamiko ya Kucheleweshwa kwa malipo ya wafanyakazi na vibarua pamoja na watoa huduma ambao wanashiriki katika ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vijijini. Tunapenda kuwafahamisha wananchi kuwa katika utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini, Wakala umeingia mikataba na wakandarasi binafsi ambao wana jukumu la kununua vifaa na kujenga miundombinu ya kusambaza umeme na wanawajibika kuwalipa vibarua pamoja na gharama nyingine zinazohitajika katika utekelezaji wa miradi husika.

Madai ya Rushwa kwa Huduma ya Kuunganisha Umeme

Aidha kumekuwepo malalamiko ua rushwa kwa huduma mbalimbali za umeme Wakala unawahimiza wananchi kuwa malipo yote ya kuunganishiwa umeme yafanyike katika ofisi za TANESCO pekee na kwamba stakabadhi zitatolewa kwa malipo hayo. Wakala unawaagiza wananchi wajiepushe kulipa fedha kwa mtu yeyote atakayewadai rushwa au kutaka malipo yoyote ya kuunganishiwa umeme yafanyike nje ofisi za  TANESCO. Aidha, Wakala unawataka viongozi pamoja na wananchi katika maeneo ya miradi kukemea na kutoa taarifa za madai ya rushwa kutoka kwa wakandarasi wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi au vibarua wao pindi yanapobainika kwenye ofisi za TANESCO, Polisi na Taasisi za Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) na vyombo vingine vya dola. Aidha, Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa wakandarasi wakubwa na wadogo, wafanyakazi na vibarua wao pindi watakapobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Kwa taarifa hii, Wakala unawaonya wakandarasi wote kutokujihusisha na vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanawadhibiti wakandarasi wadogo, wafanyakazi na vibarua wao kutokujihusisha na vitendo vya rushwa. Wakandarasi watakaoshindwa  kutekeleza agizo hili,  mikataba yao itasitishwa  na watanyimwa fursa ya kushiriki kwenye zabuni za miradi mingine ya kusambaza umeme vijijini.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S.L.P. 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Parua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007


«November 2017»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
6789101112
13

INVITATION FOR TENDER - ELECTRIFICATION OF RURAL AREAS IN SINGIDA REGION

The Rural Energy Agency invites Tenders from contractors registered with Contractors Registration Board (CRB) as Class One and Two for carrying out the Installation of Medium & Low Voltage Lines, Distribution of Transformers and Connection of Customers in Rural Areas of Singida Region.
Read more
14151617
1127

ENG. GISSIMA B. NYAMO-HANGA EMERGES THE BEST DELEGATE IN THE SUB SAHARAN AFRICA POWER SUMMIT 2017

Eng. Gissima B. Nyamo-Hanga, the Director General of Rural Energy Agency (REA - Tanzania) emerged the BEST DELEGATE in the Sub Saharan Africa Power Summit 2017 #SSAPOW17 hosted by Vale Media Group.
Read more
1819
20212223242526
27282930123
45678910