News Centre

UFAFANUZI WA REA KUHUSU TAARIFA ZILIZOTOLEWA KWENYE MAGAZETI YA JAMBO LEO NA MWANAHALISI YA IJUMAA TAREHE 15 APRILI 2016, NA HABARI LEO LA JUMAMOSI TAREHE 16 APRILI 2016

Wednesday, April 20, 2016|Number of views (1942)|Categories: News, Announcements, Press Releases

Documents to download

Wakala wa Nishati Vijijini unatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti ya Jambo Leo na Mwanahalisi ya Ijumaa Tarehe 15 Aprili 2016 pamoja na Gazeti la Habari Leo la Jumamosi Tarehe 16 Aprili 2016.

Tunapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Wakala wa Nishati Vijijini haujawahi kuingia mkataba wa kuagiza mashine-umba (Transformers) 200 kutoka TANELEC. Mashine-umba pamoja na vifaa vingine vyote vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu chini ya “Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya Pili” vinanunuliwa moja kwa moja na wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo baada ya kupewa zabuni na REA. Kwa kuwa miradi ya usambazaji umeme vijijini ina msamaha wa kodi ambao umetolewa kwa REA; kwa utaratibu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), vifaa vinaponunuliwa na mkandarasi ni lazima vioneshwe kuwa ni kwa ajili ya mradi wa REA ili viweze kupata msamaha huo wa kodi uliotolewa kwa miradi inayosimamiwa na REA.

Aidha, REA haijapeleka Mashine-umba za mradi huo unaotajwa kwa TANELEC kwa ajili ya matengenezo kama ilivyoripotiwa kwani wajibu wa kurekebisha hitilafu zozote kwenye vifaa na miundombinu inayojengwa na ambayo bado haijakabidhiwa kwa TANESCO ni la Mkandarasi. Hata baada ya kukabidhi mradi kwa TANESCO, Mkandarasi husika bado anawajibika kurekebisha kuharibika kwa vifaa na miundo-mbinu ya umeme aliyoijenga kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kukabidhi mradi kwa TANESCO kwa mujibu wa mkataba.

Aidha, kampuni ya umeme nchini TANESCO, ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa miradi iliyopo chini ya “Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini wa Awamu ya Pili”, inao wajibu wa kusimamia ubora wa vifaa na ujenzi wa miundombinu hiyo ya usambazaji umeme na kuhakikisha kuwa inajengwa kwa viwango vinavyolingana na vile vilivyofafanuliwa kwenye zabuni na mikataba. Hivyo basi; malipo yote yanayofanywa na REA kwenda kwa Wakandarasi wa miradi hiyo yanaidhinishwa na kulipwa pale tu REA inapopokea uthibitisho kutoka TANESCO kuwa kazi imefanyika kulingana na viwango vya ubora vinavyohitajika kulingana na mikataba.

Kuhusiana na masuala ya rushwa kwenye miradi; REA kupitia vyombo vya habari na kampeni za uelimishaji muda wote imesisitiza wananchi kukataa kutoa rushwa kwa ajili ya kuunganishiwa umeme na kuripoti kwenye vyombo vya dola pale wanapoombwa rushwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. REA kupitia vyombo vya habari imekuwa ikitoa maonyo kwa wakandarasi wakubwa na wadogo, wafanyakazi pamoja na vibarua wao kutojihusisha kabisa na masuala ya rushwa.

Imetolewa na:
MKURUGENZI MKUU
WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)
20 SAM NUJOMA, 14414
P. O. BOX 7990
DAR-ES-SALAAM.

Documents to download

«June 2017»
MonTueWedThuFriSatSun
2930311234
567891011
12131415

TAARIFA KWA WAKANDARASI / NOTICE TO CONTRACTORS

Wakandarasi ambao hawajakamilisha wajibu wao hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni zitakazotangazwa na Wakala.

Contractors who have not fulfilled their obligations will not be allowed to participate in the forthcoming tenders to be advertised by the Agency.
Read more
16
1113

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KITAIFA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA , BUTIAMA, MKOA WA MARA

Tarehe 5 Juni 2017, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Ulishiriki Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Butiama, Mkoa wa Mara. Wakala ulipata fursa ya kuonesha mpango wake wa kusambaza umeme vijijini.
Read more
1718
1920212223
1112

ZIARA YA VIONGOZI WA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) KATIKA WILAYA YA KILOLO

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga aliongoza ujumbe wa viongozi wa Wakala kutembelea Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa ili kutathmini matokeo chanya yaliyotokana na utekelezwaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini.
Read more
2425
26
1111

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MANYARA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Manyara uliofanyika tarehe 24/06/2017 katika kijiji cha Luxmanda, Kata ya Secheda, Wilaya ya Babati Vijijini.
Read more
2728293012
3456789