Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.
WAZIRI WA NISHATI MHE. DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA KALEMANI (MB.) AMEWASILISHA BUNGENI LEO, TAREHE 08 MEI, 2020 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2020/21
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaunga mkono juhudi za Serikali za kuchukua tahadhari dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona. Tunawaomba wadau wetu wote kushiriki pamoja katika mapambano haya.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme (TANESCO) kuweka mpango ambao utawezesha vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vinatengenezwa hapa nchini.
Uploaded is the REPDF Lot 1 Consultant Database.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. John Pombe Magufuli amemteua Wakili Julius B. Kalolo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini.
Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini imekutana wa Wakandarasi wa Mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa I katika Ukumbi wa Hazina, Dodoma kujadili changamoto mbalimbali zinazoweza kuchelewesha utekelezaji wa Mradi.