August 11 News JAPANI YAVUTIWA NA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI Serikali ya Japani imekiri kuvutiwa na kuhamasishwa na fursa za uwekezaji zilizopo hapa nchini hususan katika sekta ya nishati na imeonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo. Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan Mhe. Toshimitsu Motegi aliyasema hayo hivi karibuni alipofanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo ofisini kwake jijini Dar es Salaaam.
July 31 News PRESIDENT OBAMA TOURS SYMBION; URGES SPEED ON POWER PROJECTS United States President, Barack Obama has urged the Tanzanian government to ensure effective implementation of the electricity projects under the multi-billion dollar ‘Power Africa project’, financed by the US. President Obama made the statement during a brief visit to the Symbion Power Plant in Ubungo, Dar es Salaam early July, this year, where he launched the project.
July 16 Announcements KONGAMANO LA “BIG RESULTS NOW” MIRADI MIKUBWA YA NISHATI YATAJWA Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ametaja miradi ya kipaumbele itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa mbalimbali nchini. Prof. Muhongo aliitaja miradi hiyo mikubwa jijini Dar es Salaam mbele ya wadau waliokusanyika katika kongamano la wazi la siku moja kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
May 15 News UJERUMANI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME VIJIJINI Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na Ujerumani katika kuzalisha umeme vijijini kwa kutumia nishati mbadala hususan upepo na jua. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani.
April 13 News NORWAY YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 200 KWA AJILI YA UMEME VIJIJINI Serikali ya Tanzania imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada wa Krona milioni 700, sawa na shilingi bilioni 200 za Tanzania, kutoka Serikali ya Norway, kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini. Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisaini mkataba wenye makubaliano hayo, Aprili 9, 2013 Mjini Oslo Norway akiiwakilisha Serikali ya Tanzania, ambapo Serikali ya Norway iliwakilishwa na Waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Heikki Holmas.