Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ametaja miradi ya kipaumbele itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa mbalimbali nchini. Prof. Muhongo aliitaja miradi hiyo mikubwa jijini Dar es Salaam mbele ya wadau waliokusanyika katika kongamano la wazi la siku moja kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.