BODI YA NISHATI VIJIJINI HAIJARIDHISHWA NA KAZI YA MKANDARASI MKOA WA SINGIDA

Saturday, August 29, 2020|Number of views (3914)|Categories: News, Events
BODI YA NISHATI VIJIJINI HAIJARIDHISHWA NA KAZI YA MKANDARASI MKOA WA SINGIDA
Bodi ya Nishati Vijijini (REB) haijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini katika Wilaya ya Iramba na Mkalama mkoani Singida unayotekelezwa na Kampuni ya Emerc and Dynamic Engineering.

Mwenyekiti wa REB, Wakili Julius Kalolo alionesha wasiwasi huo kwa mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha kazi hiyo wakati Bodi yake ilipofanya ziara ya siku mbili, tarehe 26 hadi 27 Agosti 2020 ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini katika wilaya za SingidaVijijini, Iramba na Mkalama.

“Tumeona kwa kiasi fulani ametimiza maukumu yake, lakini bado yupo chini ya matarajio kwa sababu maeneo mengi hayajajengwa miundombinu ya umeme mkubwa, hata miundombinu ya umeme mdogo kwa ajili ya kuingiza majumbani hajakamilika” alisema.

Kutokana na kusuasua kwa mkandarasi huyo, Bodi ilimuagiza aongeze magenge ya kazi ili aweze kukamilisha mradi huo ifikapo tarehe 10/09/2020. Hata hivyo, Wakili Kalolo alisema mkandarasi amepewa siku tatu kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti, 2020 ambapo kama hatajirekebisha kwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi, atapunguziwa wigo wa mradi wake ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati uliopangwa.

“Atakuwa katika uangalizi wa siku tatu kama hataonesha mabadiliko atapunguziwa kazi ili asicheleweshe wananchi kupata huduma ya nishati ya umeme” alisema Wakili Kalolo.

Aidha, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu amemtaka mkandarasi kuzingatia maelekezo aliyopewa na Bodi na kutahadharisha kuwa ndani ya siku tatu kama hataonesha mabadiliko ya utendaji wake wa kazi atapunguziwa baadhi ya maeneo.

“Tumempa tahadhari baada ya siku tatu baadhi ya maeneo ambayo atakuwa hajaanza kazi TANESCO wataingia na mafundi wao kukamilisha ili wananchi waweze kuwashiwa umeme,” alisema.

Mhandisi Olotu alimuagiza mkandarasi kutumia nguvu kazi ya vijana wa vijiji ambavyo viko katika wigo wa mradi katika kazi ambazo hazihitaji utaalamu kama vile kufyeka vichaka, kuchimba mashimo na kubeba nguzo.

Akizungumza kwa niaba ya mkandarasi, Mhandisi anayesimamia mradi huo, James Kinyila alisema kuwa wamepanga magenge ya kutosha ili kukamilisha kazi hiyo kwa muda waliopewa.

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz

Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

Please login or register to post comments.

«January 2022»
MonTueWedThuFriSatSun
27
2203

MPANGO KABAMBE UPELEKAJI NISHATI VIJIJINI WABAINISHWA

Imeelezwa kuwa Mpango Kabambe wa Kupeleka Nishati Vijijini umelenga kuwanufaisha wananchi kupitia usambazaji umeme pamoja na nishati bora ya kupikia.
Read more
2829303112
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31123456