MHANDISI HASSAN SEIF SAIDY ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA REA

Thursday, September 30, 2021|Number of views (1568)|Categories: News
MHANDISI HASSAN SEIF SAIDY ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MKUU WA REA

Tarehe 25 Septemba 2021, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu alitoa taarifa kwa umma ikieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa uteuzi wa Mhandisi Said, ambaye awali alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO, umeanza tarehe 23 Septemba, 2021.

REA inatoa pongezi za dhati kwa Mhandisi Said kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kuiongoza REA. Tunaahidi kumpatia ushirikiano katika kazi yake ili azma ya Serikali ya kuwapatia wananchi wote nishati bora na ya uhakika iendelee kutekelezwa.

Aidha, tunamshukuru Mtangulizi wake, Mhandisi Amos William Maganga, kwa utumishi wake katika kuiongoza sekta husika katika kipindi chote alichotumikia kama Mkurugenzi Mkuu wa REA.

Karibu sana Mhandisi Hassan Seif Said na asante kwa utumishi wako Mhandisi Amos William Maganga. Kazi iendelee…


Please login or register to post comments.