MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI ATOA WITO KUHUSU ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI

Sunday, August 9, 2020|Number of views (4082)|Categories: News, Events, Announcements
MWENYEKITI WA BODI YA NISHATI VIJIJINI ATOA WITO KUHUSU ULINZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME VIJIJINI
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.

Wakili Kalolo alitoa wito huo tarehe 07/08/2020 alipotembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Alisema kuwa uharibifu unaofanyika katika miundombinu ya umeme ni pamoja na kuchoma moto nguzo, kuiba waya na vyuma vinavyoshikilia nguzo ili kuziwezesha ziwe imara. “Kuna watu wanaharibu miundombinu ya usambazaji wa umeme kwa kukata nyaya na vyuma vinavyofungwa katika nguzo na kutumia vifaa hivyo kufungia matela yanayokokotwa na ng’ombe” alisema.

Aidha, alitahadharisha kuwa watakaokamatwa wakiharibu miundombinu ya usambazaji wa umeme watachukuliwa hatua za kisheria na alisema kwa kuwa miundombinu hiyo inajengwa vijijini, viongozi wa vijiji wanalo jukumu la kuilinda kwa kuwashirikisha wananchi.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania

Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

«May 2022»
MonTueWedThuFriSatSun
2526272829301
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
303112345