Events

Failed to load licensing components. Please Repair / Re-Install Dixit . DO NOT UNINSTALL MODULE!

KIPAUMBELE CHA SERIKALI KATIKA KUSAMBAZA NISHATI VIJIJINI NI KUPELEKA UMEME KATIKA VITONGOJI

Monday, December 14, 2020|Number of views (3612)|Categories: News, Events
KIPAUMBELE CHA SERIKALI KATIKA KUSAMBAZA NISHATI VIJIJINI NI KUPELEKA UMEME KATIKA VITONGOJI
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Medard Kalemani amesema kipaumbele cha Serikali katika kusambaza nishati vijijini ni kupeleka umeme katika vitongoji.

Waziri Kalemani alisema hayo tarehe 11 Disemba 2020 katika ukumbi wa mikutano wa PSSF uliopo jijini Dodoma wakati akiongea na Menejimenti za Wizara ya Nishati na Taasisi zake. “Tunahitaji kupeleka umeme katika vitongoji vyote, siku hizi watu hawaulizi tena vijiji. Vitongoji viwe kipaumbele sasa” alisema.

Aidha, Mhe Waziri wa Nishati aliwapongeza REA kwa kazi nzuri ya kusambaza umeme vijijini na kuwataka wailinde imani ambayo wamepewa na wananchi kwa kuchapa kazi kwa kasi, ubunifu na usahihi. “Tunawapongeza mmefanya kazi nzuri sana, kupeleka umeme vijijini ni sacrifice, unapeleka nguzo 100 unapata wateja wanne, lakini baada ya miezi sita wateja wanaongezeka. Lazima tukubaliane kufanya kazi mara dufu ya miaka mitano iliyopita na kwa kushirikiana”, alisema.

Naye Naibu Waziri, Mhe. Stephen Byabato alisisitiza ushirikiano katika kazi na kutoa elimu kwa umma kuhusu mafanikio ya miradi inayotekelezwa na Serikali.

Baada ya kukutana na Menejimenti za Wizara ya Nishati, Waziri wa Nishati pamoja na Naibu wake walikutana na Bodi za Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ambapo katika kikao hicho, Mhe. Waziri aliagiza kila taasisi iwasilishe mpango ambao unaainisha vipaumbele, changamoto pamoja na ufumbuzi wake.

Aidha, Mhe. Waziri wa Nishati alizitaka Bodi hizo kusimamia mpango kazi huo na kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatimizi wajibu wao.

Akipokea maagizo hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo aliahidi kutoa ushirikiano kwa Waziri na Naibu wake na kuwa watahakikisha maelekezo waliyotoa yanatekelezwa.


Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz

Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

Please login or register to post comments.
«February 2023»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
6789101112
13141516171819
20212223242526
272812345
6789101112