Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Kaimu Mwenyekiti wake, Mhe. Joseph Kakunda leo, tarehe 14 Machi, 2025 imetembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya kusambaza umeme vijijini mkoani Singida kupitia Miradi ya awali kama vile REA Awamu ya Kwanza (REA I), REA Awamu ya Pili (REA II), REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza (REA III Round I), na REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round II); ambapo vijiji vyote 441 vya mkoa huo vimefikiwa na umeme huku vitongoji 1,052 vimefikiwa na huduma ya umeme kati ya vitongoji 2,289 vya mkoa wa Singida, sawa na asilimia 45.96 ya vitongoji vyote.