Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini kukamilisha kazi kwa muda waliopewa kwa mujibu wa mikataba.
Agizo hilo amelitoa leo tarehe 04 Januari, 2024 wilayani Korogwe akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili mkoa wa Tanga.
"Wanaochelewesha miradi wanawazuia wananchi kupata huduma kwa wakati kwa sababu hiyo hakuna nyongeza ya muda itakayotolewa kwa wakandarasi ambao watachelewa kukamilisha Miradi", alisema.
Aidha, Mhandisi Saidy aliwataka Wananchi kulinda miundombinu ya umeme na wakati huo huo ametoa wito kwa wananchi kutumia nishati ya umeme kuboresha vipato vyao.
Mkurugenzi Mkuu wa REA yupo mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa usambazaji nishati ya umeme katika vijiji vya wilaya ya Korogwe mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la PSSSF, Ghorofa ya 7
Barabara ya Makole
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507