Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Sasa ni Kitongoji kwa Kitongoji

Tuesday, September 29, 2020|Number of views (633)|Categories: News, Events
Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Sasa ni Kitongoji kwa Kitongoji
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Merdad Kalemani amezindua Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili tarehe 24 Septemba 2020. Mradi huu unalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji katika vijiji vilivyofikiwa na miundombinu ya umeme.

Akizindua Mradi huo katika Kitongoji cha Ufuluma Senta, Wilaya ya Uyui na Kitongoji cha Migombani, Wilaya ya Nzega, Dkt. Kalemani alisema vitongoji ambavyo havina umeme vitaanza kusambaziwa umeme sasa. “Mpango halisi wa kuanza kupeleka umeme kwenye vitongoji unaanza rasmi leo hapa Mkoani Tabora” alisema.

Alisema jumla ya vitongoji 1,103 na wateja wa awali 69,079 wataunganishiwa huduma ya umeme kwa kipindi cha miezi 9 ya utekelezaji wa Mradi huo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dr. Philemon Sengati alitoa wito kwa wananchi kutumia vizuri fursa ya upatikanaji wa huduma ya umeme ili kufanikisha malengo ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo aliwahimiza wananchi kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya kuongeza kipato kwa kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ili kubadili mfumo duni wa maisha ya vijijini.

Mradi huu unafadhiliwa na Serikli za Tanzania, Norway na Sweden pamoja na Umoja wa Ulaya kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini (REF) na utagharimu Shilingi Bilioni 142. Utatekelezwa katika mikoa tisa (9) ya Dodoma, Kilimanjaro, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Singida, Pwani, Tanga na Mbeya.

«November 2020»
MonTueWedThuFriSatSun
2627282930311
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30123456