Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yawakaribisha Wananchi Kutembelea Banda Lake Siku Ya Chakula Duniani Tanga
Mohamed Saif 0

REA Yawakaribisha Wananchi Kutembelea Banda Lake Siku Ya Chakula Duniani Tanga

REA kuonesha mchango wa nishati katika kukuza kilimo na uzalishaji wa chakula

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unawakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda lake katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Chakula Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Usagara, Tanga Mjini, kuanzia Oktoba 10 hadi 16, 2026

Maadhimisho hayo yamefunguliwa rasmi  Oktoba 12, 2026, na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, yakiongozwa na kaulimbiu *“Ubunifu wa Leo, Lishe Bora ya Kesho: Kuelekea Dira 2050.”

Ushiriki wa REA unalenga kuonesha mchango wa nishati katika kuimarisha shughuli za kilimo, uzalishaji, uchakataji na uhifadhi wa mazao, kuongeza tija na kuchochea maendeleo ya kiuchumi vijijini.

Katika banda la REA, wananchi watapata fursa ya kuzungumza na wataalamu wa Wakala, kupata elimu kuhusu miradi ya umeme vijijini, nishati jadidifu, nishati safi ya kupikia na matumizi ya nishati katika shughuli za uzalishaji na biashara.

REA inawakaribisha wakulima, wafanyabiashara, wananchi na wadau wote kutembelea banda lake katika Viwanja vya Usagara, Tanga Mjini, kujifunza na kufahamu fursa za nishati zinazoweza kuongeza tija, kukuza uchumi na kuboresha maisha. 

 

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top