Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo Mwaka 2030
Mohamed Saif 166

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo Mwaka 2030

“Tumebeba Matumaini ya Wananchi” — Mha. Saidy

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, amesema Serikali imedhamiria kukamilisha miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vyote ifikapo mwaka 2030, hatua ambayo itachochea shughuli za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.

Mha. Saidy ameyasema hayo Septemba 22, 2026 jijini Dodoma, wakati akizungumza katika Kikao Kazi cha Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu, maendeleo ya miradi pamoja na kuimarisha usimamizi ili kuhakikisha malengo ya Wakala yanafikiwa kwa wakati.

Akisisitiza umuhimu wa wajibu walio nao watumishi katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kufikisha nishati vijijini, Mha. Saidy amesema, “Tumebeba matumaini ya wananchi,” akiwataka watumishi kutambua kuwa mafanikio ya miradi yanagusa moja kwa moja maisha na shughuli za maendeleo za wananchi.

Aidha, Mha. Saidy amewataka wasimamizi wa miradi kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu, sambamba na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi katika maeneo yao na kuhakikisha changamoto zinazoweza kuchelewesha miradi zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Amesisitiza kuwa ushirikiano, ufuatiliaji madhubuti na uwajibikaji wa kila mtumishi ni muhimu katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa na kukamilika kwa wakati, ili wananchi waweze kunufaika na huduma ya umeme na kuitumia katika shughuli za uzalishaji na maendeleo.

Kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, REA inaendelea kuimarisha juhudi za Serikali za kupanua wigo wa upatikanaji wa nishati vijijini, huku ikihimiza matumizi yenye tija ya umeme ili huduma hiyo iwe chachu ya kuinua uchumi wa wananchi na kuharakisha maendeleo katika maeneo ya vijijini.

Share

Print
«November 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
26
REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

Wananchi wanaoishi katika Visiwa wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia mifumo ya umeme jua kwa bei ya ruzuku hali iliyosaidia kuboresha maisha yao visiwani.

Pongezi hizo zimetolewa leo na wananchi wanaoishi katika Kisiwa cha Bezi kilichopo katika Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ilipotembelea kisiwani hapo kuona maendeleo ya mradi huo ambao unafadhiliwa na benki hiyo na kusimamiwa na REA katika visiwa 120 nchini.

Read more
2728
REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Read more
2930
Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Benki ya Dunia yapongeza miradi ya umeme vijijini kwa kuboresha maisha ya wananchi vijijini pamoja na huduma za kijamii.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mtaalam Mwandamizi wa Fedha kutoka Benki ya Dunia, Nkundwe Mwakiluma wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia iliyolenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
311
23
The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey provides data to inform energy-related programs and projects.

Read more
45678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top