Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yatoa Somo La Nishati Safi Ya Kupikia Kwa Vitendo Nanenane
Mohamed Saif 160

REA Yatoa Somo La Nishati Safi Ya Kupikia Kwa Vitendo Nanenane

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bi. Martha Chassama, ameendelea kutoa elimu kwa vitendo kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuandaa na kupika vyakula kwa kutumia majiko ya kisasa yanayotumia nishati safi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za uelimishaji wa wananchi wanaotembelea banda la REA katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya onesho hilo, Bi. Chassama amesema REA inaendelea kutekeleza kwa kasi miradi ya nishati safi ya kupikia nchini kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa nishati salama, nafuu na rafiki kwa mazingira, sambamba na kuboresha afya za wananchi na kuhifadhi mazingira.

“Nishati safi ya kupikia siyo tu suluhisho la kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, bali ni uwekezaji katika afya za wananchi, uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya uchumi wa familia. REA inaendelea kuhakikisha wananchi wanapata elimu na fursa ya kutumia teknolojia hizi za kisasa ili kuboresha maisha yao,” amesema Bi. Chassama.

Amefafanua kuwa maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kujionea kwa vitendo namna majiko ya kisasa yanavyofanya kazi, kufahamu manufaa yake pamoja na kupata elimu kuhusu teknolojia mbalimbali za nishati safi ya kupikia zinazotekelezwa na REA kwa kushirikiana na Serikali na wadau wa maendeleo.

Aidha, amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia yanachangia kupunguza athari za kiafya zitokanazo na moshi wa kuni na mkaa, kulinda mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti, pamoja na kuokoa muda na gharama zinazotumika katika kutafuta nishati za kupikia.

Bi. Chassama amewahimiza wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane kutembelea banda la REA ili kupata elimu kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, nishati safi ya kupikia na teknolojia za nishati jadidifu, zinazolenga kuboresha maisha ya Watanzania na kuchochea maendeleo endelevu.

Maonesho ya Nanenane ya mwaka 2026 yanaendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, yakitoa jukwaa kwa taasisi za umma na sekta binafsi kuonesha huduma, ubunifu na teknolojia zinazochangia maendeleo ya sekta ya kilimo na uchumi wa Taifa. 

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top