NORWAY YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 200 KWA AJILI YA UMEME VIJIJINI
Serikali ya Tanzania imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada wa Krona milioni 700, sawa na shilingi bilioni 200 za Tanzania, kutoka Serikali ya Norway, kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini. Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisaini mkataba wenye makubaliano hayo, Aprili 9, 2013 Mjini Oslo Norway akiiwakilisha Serikali ya Tanzania, ambapo Serikali ya Norway iliwakilishwa na Waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Heikki Holmas.
Read more