Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Umeme Kubadilisha Maisha Ya Wananchi Vitongojini
Mohamed Saif 326

Umeme Kubadilisha Maisha Ya Wananchi Vitongojini

Serikali imedhamiria kubadilisha maisha ya wananchi vitongojini kupitia usambazaji wa umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wananchi wamehimizwa kuchangamkia kuunganishiwa umeme kwenye vitongoji vilivyofikiwa.

Hayo yamesemwa Julai 15, 2026 na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kitongoji cha Mwamlula katika Kijiji cha Mseko na Kitongoji cha Kipeke katika Kijiji cha Masagi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ameuwezesha Wakala wa Nishati Vijijini kuweza kutekeleza majukumu yake kisawasawa na anaendelea kuiwezesha ili kutimiza azma ya kuwafikishia maendeleo wananchi vijijini na vitongojini,” amesema Balozi Kingu.

Amesema mpango uliopo ni kuhakikisha umeme unafika katika vitongoji vyote 64,359 ifikapo Mwaka 2030 na kuwa hadi sasa asilimia 62.4 ya vitongoji tayari vimefikiwa na kwamba hakuna shaka kwa uwezeshwaji unaotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mpango huo utafikiwa kikamilifu.

Amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanatumia umeme kubadilisha maisha yao ya kila siku kama ilivyo azma ya Serikali kwa kuanzisha miradi na shughuli mbalimbali ya kiuchumi kwani umeme ni fursa ya kubadilisha maisha.

“Mnaweza kubadilisha maisha yenu ya kila siku mkaongeza mapato ya kiuchumi kutokana na kufikiwa na umeme kwani pia huduma zingine za kijamii zinazotegemea umeme zitaanzishwa na zingine lkuendelezwa,” amesema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Thomas Mbaga akizungumza katika hafla hiyo amesema mkoa wa Singida una jumla ya vitongoji 2,289, kati ya hivyo vitongoji 1,196 sawa na 52.25% tayari vimeunganishwa na huduma ya umeme, huku vitongoji 1,093 sawa na 47.75% bado havijafikiwa na huduma hiyo na kwamba utekelezaji wa miradi unaendelea kupitia miradi ya HEP IIA itakayofikisha umeme katika vitongoji 127 na HEP IIB vitongoji 377.

Mha. Mbaga amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanalinda na kutunza miundombinu kwani Serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza miradi ya kusambaza umeme na huku akitolea mfano kwa Mkoa wa Singida pekee kuwa hadi sasa takriban shilingi bilioni 94.6 zimetumika kutekeleza miradi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa vitongoji vya Mwamlula na Kipeke wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia umeme na wamebainisha namna ambavyo unakwenda kubadilisha maisha yao.

“Tumefurahi kufikishiwa umeme, ilikuwa ni kama ndoto tu lakini leo hii tumeshuhudia umeme umewashwa na tutajitahidi kuhakikisha tunautumia pia kujiongezea kipato mbali na kutuangazia wakati wa usiku,” amesema Lucia Constantine mkazi wa kitongoji cha Mwamlula.

 

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top