Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Yaridhishwa na Usambazaji wa Umeme Kisiwani Jibondo
Newsletters

Bilioni 8 zatumika

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Yaridhishwa na Usambazaji wa Umeme Kisiwani Jibondo

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imeeleza kuridhishwa kwake na kasi ya usambazaji wa nishati ya umeme katika vitongoji vya Kisiwa cha Jibondo, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, mkoani Pwani.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa REB, Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu, tarehe 27 Agosti, 2026 alipoambatana na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kisiwani humo kukagua maendeleo ya mradi huo mkubwa ambao tayari umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meja Jenerali Kingu amesema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia, vitongoji vya Kisiwa cha Jibondo vinatarajia kupata huduma hiyo ya nishati hivi karibuni. Alifafanua kuwa kazi kubwa iliyobaki kwa sasa ni ya usafirishaji wa umeme kwa kutumia waya maalum wa chini ya maji (Submarine cable) kutoka kisiwa kidogo cha Juani kwenda Jibondo, kazi inayotarajiwa kuanza kesho, tarehe 29 Agosti 2026, na kukamilika baada ya siku tano.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy, amesema kuwa maandalizi yote ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa njia za kusafirisha umeme ndani ya kisiwa hicho yamekamika kwa asilimia 90 na ameongeza kuwa mara baada ya nyaya hizo za chini ya maji kuunganishwa, wananchi wataanza kuunganishiwa huduma hiyo mara moja.

Mhandisi Saidy amebainisha kuwa mradi huo umefanikiwa kwa ushirikiano wa REA iliyochangia shilingi bilioni 6.8 na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lililochangia shilingi bilioni 2.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Saidy ametoa wito kwa wakazi wa Jibondo kujiandaa kiuchumi ili kuutumia umeme huo katika kuboresha maisha yao na kuendesha shughuli za kimaendeleo, hasa ikizingatiwa kuwa sehemu kubwa ya wakazi wa eneo hilo wamejiajiri kwenye sekta za uvuvi, usindikaji wa mazao ya bahari, na kilimo cha mwani.

Wilaya ya Mafia ina jumla ya vitongoji 136, ambapo vitongoji 111 tayari vimeshafikishiwa huduma ya umeme. Vitongoji vingine 19 vipo kwenye mpango wa utekelezaji kupitia Mradi wa HEP II (B), huku vitongoji 6 vilivyobaki vikiwa ni hivyo vya Kisiwa cha Jibondo vinavyosubiri kuwashwa kwa umeme huo hivi karibuni.

Naye mmoja wa wakazi wa kisiwa hicho, Mzee Abdalah Hassan, ameishukuru Serikali kwa uwekezaji huo mkubwa na kueleza kuwa umeme huo utakuwa mkombozi mkubwa kwao.

"Umeme unahitajika kila mahali. Shuleni utasaidia kuchapisha mitihani na kujifunza kwa njia ya kompyuta, lakini pia utatupa wepesi wa kuandaa chakula na kuleta mwanga majumbani. Tumefarijika sana, ni faraja kubwa isiyo na kifani," amesema Mzee Abdalah.

-         MWISHO –

 

 

REA Yaanza Ujenzi Wa Vituo Vidogo Vya Mafuta Vijijini
News

REA Yaanza Ujenzi Wa Vituo Vidogo Vya Mafuta Vijijini

Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Advera Mwijage, amesema REA imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa vituo vidogo vya mafuta vijijini ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mafuta na kuchochea maendeleo ya shughuli za kiuchumi katika maeneo ya vijijini.
 

REA Yatoa Somo La Nishati Safi Ya Kupikia Kwa Vitendo Nanenane
News

REA Yatoa Somo La Nishati Safi Ya Kupikia Kwa Vitendo Nanenane

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Bi. Martha Chassama, ameendelea kutoa elimu kwa vitendo kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kuandaa na kupika vyakula kwa kutumia majiko ya kisasa yanayotumia nishati safi, ikiwa ni sehemu ya shughuli za uelimishaji wa wananchi wanaotembelea banda la REA katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
 

Umeme Kubadilisha Maisha Ya Wananchi Vitongojini
News

Umeme Kubadilisha Maisha Ya Wananchi Vitongojini

Serikali imedhamiria kubadilisha maisha ya wananchi vitongojini kupitia usambazaji wa umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na wananchi wamehimizwa kuchangamkia kuunganishiwa umeme kwenye vitongoji vilivyofikiwa.

RSS
1345678910Last
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top