Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa  Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za  Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini
Announcements

Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini unakaribisha maombi ya mkopo nafuu kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kuuzia bidhaa za mafuta (petroli na dizeli) vijijini. Mkopo huu utasaidia uwezeshaji wa ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa gharama nafuu, kwa njia salama, na isiyo na madhara kwa mazingira.

Wakala unawasisitiza waombaji walioomba katika awamu ya kwanza na kutokidhi vigezo kuomba tena baada ya kufanya marekebisho  ya  mapungufu yaliyobainishwa katika maombi yao. Aidha maombi mapya ya mkopo yanakaribishwa.

Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu Ameteuliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB)
Announcements

Raisi Avunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini REA, Leo Tarehe 25 Septemba 2023

Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu Ameteuliwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassam amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kumteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Nishati Vijijini (REB) ambayo inasimamia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo tarehe 25 Septemba 2023.

Rais Samia Awaapisha Waziri na Naibu Waziri wa Nishati
News

Rais Samia Awaapisha Waziri na Naibu Waziri wa Nishati

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 1, 2023 amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni (Agosti 30, 2023) kushika nyadhifa mbalimbali akiwemo Mhe. Dkt. Doto Biteko kwa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu (Uratibu wa Shughuli za Serikali) na Waziri wa Nishati pamoja na Mhe. Judith Kapinga kwa nafasi ya Naibu Waziri wa Nishati.

REA yawaneemesha wananchi kwa kukamilisha kituo cha kupoza umeme Ifakara
News

REA yawaneemesha wananchi kwa kukamilisha kituo cha kupoza umeme Ifakara

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekamilisha Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme kilichopo Ifakara (Ifakara Substation) na kuleta neema ya umeme wa uhakika kwa wananchi wa wilaya za Kilombero na Ulanga mkoani Morogoro, ambao walikuwa na changamoto ya kupata umeme mdogo na wenye kukatika mara kwa mara.

MAONESHO YA SABASABA MWAKA 2023
News

NISHATI YA KUPIKIA NI SEHEMU YA VIPAUMBELE VYA KITAIFA

MAONESHO YA SABASABA MWAKA 2023

Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA); Mhandisi, Francis Songela amesema Serikali kupitia REA imetoa kipaumbele kwenye kuongeza matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia na kuongeza kuwa Wananchi wanapaswa kuchangamkia teknolojia mbalimbali kwa kuwa suala hilo lipo kwa ajili ya kulinda afya za Watu, kuboresha maisha yao hususan kwa Wananchi wa vijijini.

RSS
1345678910Last
«March 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
26272829123
45678910
11121314151617
18192021222324
25
Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa  Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za  Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini unakaribisha maombi ya mkopo nafuu kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kuuzia bidhaa za mafuta (petroli na dizeli) vijijini. Mkopo huu utasaidia uwezeshaji wa ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa gharama nafuu, kwa njia salama, na isiyo na madhara kwa mazingira.

Wakala unawasisitiza waombaji walioomba katika awamu ya kwanza na kutokidhi vigezo kuomba tena baada ya kufanya marekebisho  ya  mapungufu yaliyobainishwa katika maombi yao. Aidha maombi mapya ya mkopo yanakaribishwa.

Read more
262728293031
1234567

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
PSSSF Building, 7th Floor
Makole Road
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top