Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Nishati Vijijini (REA) inayotekelezwa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kwa upande wa REA ziara hiyo imehitimishwa katika kijiji cha Welela, Jimbo la Lupembe, ambapo kamati hiyo imepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa vijijini kwa kasi inayostahili.