Serikali kupitia Wakala na Mfuko wa Nishati Vijijini (REA/REF) inafadhili miradi ya kusambaza umeme vijijini katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Miradi ya Awamu ya Pili ya Usambazaji Umeme Vijijini inatekelezwa na wakandarasi kutoka sekta binafsi ambao uhusika na ujenzi wa miundombinu.