Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
BODI YA WAKURUGENZI YA REA WAKUTANA NA WAKANDARASI, PAMOJA NA WATENGENEZAJI WA VIFAA VYA MRADI WA UMEME VIJIJINI
Admin.Frank Mugogo 10113

BODI YA WAKURUGENZI YA REA WAKUTANA NA WAKANDARASI, PAMOJA NA WATENGENEZAJI WA VIFAA VYA MRADI WA UMEME VIJIJINI

1. Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini leo tarehe 08 Juni 2019 imekutana wa Wakandarasi wa Mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa I katika Ukumbi wa Hazina, Dodoma kujadili changamoto mbalimbali zinazoweza kuchelewesha utekelezaji wa Mradi. Pia Menejimenti ya REA ilishiriki mkutano huo. Mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa I unagharimu Shilingi Trilioni 1.2, ukiwa ni mradi mkubwa kusini mwa jangwa la Sahara ambapo vijiji 3,559 vitaunganishwa na huduma ya nishati ya umeme nchi nzima.

2. Bodi ya Wakurugenzi ilitaka kujua mahusiano mazuri kati ya Wakandarasi wa Mradi huo pamoja na watengenezaji wa vifaa vya mradi kama vile nguzo, nyaya, transfoma, mita na vifaa vingine. Mahusiano mazuri kati ya Wakandarasi wa watengenezaji vifaa hivyo yanaleta tija katika kuharakisha utekelezaji wa mradi.

3. Wakandarasi walieleza baadhi ya changamoto kuhusu kuchelewa kupata vifaa wanavyoagiza kutoka kwa watengenezaji. Bodi ilielezwa na watengenezaji wa vifaa hivyo kuwa wanavyo vya kutosha na watarekebisha kasoro zozote zilizojitokeza ili kuwawezesha Wakandarasi kukamilisha utekelezaji wa Mradi kwa wakati.

4. Bodi, baada ya kuwasikiliza Wakandarasi pamoja na watengenezaji wa vifaa vya mradi, ilieleza kuwa changamoto zilizoelezwa ziko ndani ya uwezo wa kutatuliwa. Changamoto kubwa iliyoonekana ilikuwa ni uelewa wa baadhi ya taratibu ikiwemo bondi inayowekwa na Benki.

5. Mkutano ulisisitiza kuwa Mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa I utakamilika ifikapo Desemba, 2019 na Wakandarasi atakayechelewesha Mradi kwa mujibu wa Mkataba hawatavumiliwa.

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

E-Mail: info@rea.go.tz
Tel: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top