Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ametaja miradi ya kipaumbele itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa mbalimbali nchini. Prof. Muhomgoaliitaja miradi hiyo mikubwa jijini Dar es Salaam mbele ya wadau waliokusanyika katika kongamano la wazi la siku moja kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
Prof. Muhongo alitoa changamoto kwa wananchi la kumchukulia hatua yeye na watendaji walio chini ya wizara yake, endapo watashindwa kulifikia lengo hilo. Alisema Wizara imedhamiria kuhakikisha miradi hiyo kwa kipindi hicho, inaleta matokeo muafaka ‘big result now’ yatakayoonekana wazi kwa Watanzania wote.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim Maswi alisema Watanzania watarajie mambo makubwa kutokana na miradi hiyo ambayo itapelekea kumaliza tatizo la umeme nchini.
Kiambatanisho: Taarifa ya Uchambuzi na Mapendekezo ya Utekelezaji wa Miradi Yenye Lengo la Kuleta Matokeo Makubwa Sasa Kwa Wizara ya Nishati na Madini.
Taarifa ya kimaabara inayoelezea kwa kina uchambuzi wa miradi ya kipaumbele ya nishati iliyotokana na upembuzi wa kimaabara uliofanyika kwa kipindi cha wiki sita (6), kuanzia tarehe 22 Februari hadi tarehe 5 Aprili 2013. Utekelezaji wa miradi hii unaanza rasmi tarehe 1 Julai 2013 na wizara ina jukumu la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi hii kama ilivyopangwa pamoja na kutatua matatizo yote yanayoweza kukwamisha utekelezaji wa miradi hiyo kukamilika mapema zaidi. Miradi hiyo yote inapaswa kukamilika utekelezwaji wake ifikapo mwezi Juni, 2016.
Imeandaliwa na:
Mohamed M. Saif
Afisa Habari
Wizara ya Nishati na Madini
754/33, Samora Avenue
S. L. P. 2000
Dar es Salaam, Tanzania
info@mem.go.tz
www.mem.go.tz