Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mkurugenzi Mkuu wa REA Akagua Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupozea Umeme Ifakara
Aodax K. Nshala 782

Mkurugenzi Mkuu wa REA Akagua Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Kupozea Umeme Ifakara

Kitakuwa na uwezo wa MVA 20 na kitasaidia wananchi Kilombero, Ulanga na Malinyi

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema ujenzi wa mradi wa kituo cha kupooza na kusambaza umeme Ifakara kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha MVA 20 kitasaidia wananchi wa wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi kupata huduma bora ya umeme na ya uhakika.

Kituo cha kupoza umeme cha Ifakara kilichoanza kujengwa Machi 2020, kinatarajiwa kuhudumia Wananchi wa wilaya za Kilombero na Ulanga kwa ufanisi mkubwa na kupunguza kwa sehemu kubwa changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Hayo yamesemwa tarehe 8 Disemba, 2022 katika mji wa Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Saidy alipozungumza na Wanahabari kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo hicho ambao aliuelezea kuwa umeongeza kilomita 82 za miundombinu ya usambazaji wa umeme katika Wilaya ya Kilombero na Ulanga.

Mhandisi Saidy amesema kuwa, ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 80.1 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2023 ambapo mpaka sasa tayari transfoma ya kisasa imeshawekwa na kituo kitatoa njia nne za umeme ambazo zitapeleka nishati hiyo kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hizo.

Akizungumza kuhusu kurefusha njia za kusambaza umeme, Mhandisi Saidy amesema, mradi huo umeshakamilika na njia hizo zenye jumla ya kilomita 82 zitaweza kufikia vijiji na vitongoji takribani 15 katika wilaya ya Kilombero.

"Kwa muda mrefu wananchi wa maeneo haya walikuwa wanapata changamoto ya kukatika kwa umeme na kupungua kwa nguvu ya umeme ambayo imesababisha kuunguza vifaa vya umeme na hata mitambo, hivyo Mradi huu utaondoa adha ya umeme kukatika na utaboresha ubora wa huduma," alisema.

Mradi huo wa kituo cha kupoza umeme na kilomita 82 za miundombinu ya usambazaji wa umeme vinagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa

kushirikiana na Jumuiya ya Ulaya kwa gharama ya EURO milioni 8.75 ambapo Kituo cha kupoza umeme pekee kimegharimu EURO milioni 5.4.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bwana Gerson Msigwa, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo, Bwana Rodney Thadeus amesema kuwa nishati inafungamanisha na maendeleo mengine ya kiuchumi ambapo Serikali imeendelea kujenga miundombinu mbalimbali ikiwemo hospitali na shule pamoja na kuwawezesha wakulima, hivyo ukosefu wa nishati utafanya shughuli hizo kutokwenda vizuri.

"Natoa rai kwa Wananchi kushirikiana na Serikali katika kuibadilisha Tanzania kupitia REA ambayo inaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania kwa kuhakikisha wanapata nishati," alikaririwa Bwana Thadeus.

Rate article

No rating
Rate this article:
No rating

Share

Print
«July 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
24252627282930
1234
National Clean Cooking Strategy (2024 – 2034)

National Clean Cooking Strategy (2024 – 2034)

The Government of the United Republic of Tanzania, in collaboration with various stakeholders has prepared the National Clean Cooking Strategy. The strategy aims to ensure that 80 percent of Tanzanians use clean cooking solutions by the year 2034.

Read more
567
891011121314
15161718192021
Vijiji 151 Vimebaki Nchi Nzima Kupata Huduma ya Umeme – Kapinga

Vijiji 151 Vimebaki Nchi Nzima Kupata Huduma ya Umeme – Kapinga

Ni vijiji 151 tu nchi nzima ndio ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme kati ya Vijiji zaidi ya 12,000 ambapo wilayani Ludewa mkoani Njombe vimebaki Vijiji nane.

Read more
22232425262728
2930311234

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
PSSSF Building, 7th Floor
Makole Road
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top