Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA: Usambazaji Wa Umeme Waendelea Kufungua Fursa Za Uzalishaji, Ajira Na Maendeleo Vijijini
Mohamed Saif 204

REA: Usambazaji Wa Umeme Waendelea Kufungua Fursa Za Uzalishaji, Ajira Na Maendeleo Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), umesema usambazaji wa umeme vijijini unaendelea kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kufungua fursa za uzalishaji, ajira na uwekezaji, huku ukiboresha maisha ya wananchi kupitia maendeleo ya sekta mbalimbali za kiuchumi.

Akizungumza katika Maonesho ya Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mha. Jones Olotu, amesema uwekezaji wa Serikali kupitia REA katika miradi ya kusambaza umeme; umewezesha sekta mbalimbali za uzalishaji kukua kwa kasi na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa vijijini.

“Lengo la REA si kusambaza umeme pekee yake bali kuhakikisha umeme unakuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwezesha viwanda vidogo na vya kati, biashara, huduma za kijamii pamoja na shughuli nyingine za uzalishaji vijijini,” amesema Mha. Olotu.

Ameeleza kuwa upatikanaji wa umeme wa uhakika umeongeza tija katika shughuli za uzalishaji, umeimarisha mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo kupitia uchakataji, uhifadhi na uongezaji thamani, hatua inayowawezesha wakulima na wajasiriamali kuongeza kipato na ushindani wa bidhaa zao sokoni.

Aidha, amesema maendeleo hayo yameongeza fursa za ajira, kuchochea uwekezaji katika viwanda vidogo na vya kati, kukuza biashara na kuboresha utoaji wa huduma muhimu za kijamii, ili kuimarisha ustawi wa wananchi na uchumi wa vijijini kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa REA itaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme na kuwaunganisha wananchi na huduma hiyo ili kuhakikisha nishati ya umeme inaendelea kuwa nguzo muhimu ya maendeleo endelevu na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Aidha, wananchi wanaotembelea banda la REA katika Maonesho ya Nanenane wanaendelea kujifunza kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na namna huduma hiyo inavyoendelea kufungua fursa za kiuchumi, kuongeza tija katika uzalishaji na kubadilisha maisha ya Watanzania.

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top