Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini
Issa Sabuni 229

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Uwekezaji huo mkubwa unatajwa kuwa si tu utasaidia kuongeza umeme katika Gridi ya Taifa, bali pia utafungua fursa za ajira, kuongeza mzunguko wa fedha, na kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi kwenye jamii zinazozunguka miradi hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya waendelezaji wadogo, Joseph Chome kutoka mradi wa Maporomoko ya Ruswisi, alisema REA imekuwa nguzo muhimu katika hatua za uanzishwaji wa miradi ikiwemo uandaaji wa upembuzi yakinifu (Feasibility Study) ambao unagharimu fedha nyingi.

Chome alipongeza mafunzo ya nadharia na vitendo yaliyotolewa na REA kwa kushirikiana na Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mjini Iringa, akibainisha kuwa yamewasaidia kupata uelewa mpana wa kitaalamu tofauti na awali ambapo wengi walikuwa wakifanya kazi kwa kubahatisha.

Katika hatua nyingine, waendelezaji hao walipata nafasi ya kutembelea mradi kufua umeme wa maporomoko ya maji wa Maguta uliopo katika kata ya Maguta, wilayani Kilolo na unamilikiwa na kampuni ya Lung’ali Natural Resource Ltd; chini ya Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa na umefikia asilimia 95 ya utekelezaji wake baada ya kuwezeshwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 1 na REA.

Msimamizi wa mradi huo, Padri Lucian Mpoma, alishukuru Serikali kwa uwezeshaji huo na kueleza kuwa mradi huo utazalisha megawati 2.4 zitakazoingizwa kwenye gridi ya taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

"Maandalizi yalianza tangu mwaka 2010 kwa kutengeneza mpango wa biashara na kushirikisha wananchi. Hivi sasa miundombinu yote muhimu ikiwemo transfoma na njia za umeme imekamilika. Tunatarajia kuanza majaribio mwezi huu wa Septemba 2026, na uzinduzi rasmi utafanyika mwezi Oktoba," alisema Padri Mpoma.

Naye Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisisitiza kuwa wakala huo utaendelea kutoa elimu, msaada wa kuandaa maandiko ya biashara, na tathmini ya mazingira kwa waendelezaji wa nishati jadidifu ikiwemo umeme wa maji na jua ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa.

Serikali imefadhiri na kuwezesha miradi kadhaa maeneo ya Nyanda za Juu Kusini; ambapo REA ilitoa kati ya shilingi bilioni 5.4 kufadhili mradi wa Lupali uliopo mkoani Njombe, mradi unaoendeshwa na Shirika la Masista wa Convent ya Mtakatifu Gertrud Imiliwaha.

Mradi mwengine wa kufua umeme kwa njia ya maporomoko ya maji ni pamoja na mradi wa Mwenga Hydro, uliounganisha wateja takriban 8,000, huku ruzuku nyengine iliyotolewa na REA ikiongeza wateja 2,900.

- MWISHO –

 

Share

Print
«November 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
26
REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

Wananchi wanaoishi katika Visiwa wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia mifumo ya umeme jua kwa bei ya ruzuku hali iliyosaidia kuboresha maisha yao visiwani.

Pongezi hizo zimetolewa leo na wananchi wanaoishi katika Kisiwa cha Bezi kilichopo katika Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ilipotembelea kisiwani hapo kuona maendeleo ya mradi huo ambao unafadhiliwa na benki hiyo na kusimamiwa na REA katika visiwa 120 nchini.

Read more
2728
REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Read more
2930
Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Benki ya Dunia yapongeza miradi ya umeme vijijini kwa kuboresha maisha ya wananchi vijijini pamoja na huduma za kijamii.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mtaalam Mwandamizi wa Fedha kutoka Benki ya Dunia, Nkundwe Mwakiluma wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia iliyolenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
311
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top