Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaanza Kusambaza Umeme Vitongoji Morogoro
Frank A. Mugogo 159

REA Yaanza Kusambaza Umeme Vitongoji Morogoro

Serikali kupitia Wakala  wa Nishati Vijijini (REA) imeanza kusambaza Umeme kwenye Vitongoji 166 vilivyopo Mkoa wa Morogoro baada ya kukamilisha nishati hiyo kwenye Vijiji 652 kati ya 669  sawa na Asilimia 97.5.
 
Mradi huo wenye gharama ya shilingi bilioni 17.9 unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miezi 24 na utakapokamilika utanufaisha zaidi ya Kaya 5,478.
 
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha Mkandarasi huyo ambaye ni kampuni ya SINOTEC CO. LTD, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo pamoja na kuwapongeza REA kwa kusimamia vyema maono ya Mhe. Rais kuhakikisha wananchi vijijini nao wanapata maendeleo kupitia upatikanaji wa nishati ya umeme.
 
“Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa kimkakati, Mkoa wa uzalishaji na tumejipanga kuwa Mkoa namba moja katika kilimo nchini. Na kuwepo kwa umeme maeneo ya vijijini kutasaidia kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Umeme ndio nguzo namba moja katika kuongeza thamani mazao ya kilimo. Tuendelee kumpongeza na kumshkuru Mhe. Rais kwa kutoa fedha zinazoenda kuwezesha zaidi ya Vitongoji 166 vinapata umeme,” amesema Mhe. Malima.
 
Mhe. Malima pia ameendelea kuwasisitiza wananchi kutunza miundombinu ya umeme na kumtaka pia mkandarasi huyo kuhakikisha anatekeleza mradi huo ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango vya ubora vinavyokubalika.
 
Awali akitoa taarifa ya upelekaji wa umeme Vijijini, Mhandisi Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Kati, Mhandisi Aneth Malingumu amesema kuwa kati ya Vijiji 669 katika Mkoa wa Morogoro, Vijiji 652 ambavyo ni sawa na asilimia 97.5 vimefikiwa na nishati ya umeme na kuongeza kuwa vijiji 17 vilivyobaki viko kwenye hatua za miwisho za ukamilishaji na kabla ya Oktoba 20 vitakuwa vimepata umeme.
 
Kwa upande wa Vitongoji, Mhandisi Malingumu amesema kuwa Mkoa wa Morogoro unajumla ya Vitongoji 3,369 na katika hivyo, Vitongoji 1,655 sawa na asilimia 49 tayari vimepatiwa umeme.
 
“Katika kipindi cha miaka miwili tunategemea vitongoji 455 vya Mkoa wa Morogoro vitapatiwa umeme. Ndani ya hivyo, 289 mkandarasi tayari yuko site na anaendelea na kazi kupitia mradi wa ujazilizi yaani Densification IIB. Aidha, vitongoji 166 vitapatiwa umeme kupitia mradi huu tunaotambulisha mkandarasi wake leo kwa gharama ya shilingi Bilioni 17.9.” Amefafanua Mhandisi Malingumu.
 
Mhandisi Malingumu pia amemuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa REA imejipanga vyema kuhakikisha umeme unafika kwenye vijiji vyote na safari ya kupeleka umeme katika vitongoji inaendelea kulingana na upatikanaji wa fedha.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kampuni SINOTEC CO. LTD, Zhang Jianguang ameahidi kutekeleza mradi huo kwa wakati na kwa ubora na kwamba tayari ameanza maandalizi yote muhimu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la REA
Mtaa wa Medeli
P. O. Box 2153,
DODOMA, TANZANIA.

Share

Print
«March 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526272812
3456
Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Arusha Wavutiwa na Bidhaa za Nishati Safi ya Kupikia

Wananchi Jijini Arusha wamevutiwa na bidhaa mbalimbali za Nishati Safi ya Kupikia na wameipongeza Serikali kwa kuona umuhimu wa kufikisha bidhaa hizo katika Maonesho yanayoendelea mkoani humo kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.

Read more
789
10
Watumishi Wanawake REA Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Arusha

Watumishi Wanawake REA Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Jijini Arusha

Watumishi Wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wameshiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kitaifa Jijini Arusha Machi 8, 2025.

Read more
111213141516
171819
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yahitimisha Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme Mkoani Njombe

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yahitimisha Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme Mkoani Njombe

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Nishati Vijijini (REA) inayotekelezwa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kwa upande wa REA ziara hiyo imehitimishwa katika kijiji cha Welela, Jimbo la Lupembe, ambapo kamati hiyo imepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa vijijini kwa kasi inayostahili.

Read more
20212223
24252627282930
31123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top