Wakala wa Nishati Vijijini (REA) itashiriki katika Maonesho ya Samia KILIMO Biashara Expo 2024 kwa msimu wa tatu yanayotarajiwa kuanza tarehe 6 Oktoba, 2024 wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Teknolojia Mbadala na Nishati Jadidifu, Mha. Advera Mwijage amesena kupitia maonesho hayo yatawawezesha wananchi kujadiliana kuhusu matumizi ya Nishati Safi na Fursa ya Biashara ya Kaboni ambapo Wizara ya Nishati kupitia REA itagawa mitungi ya gesi na majiko banifu kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabri Makame amesema wananchi hao wanakwenda kushuhudia mageuzi makubwa ya utunzaji wa mazingira kupitia Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema Gairo inatekeleza kampeni ya URITHI WA KIJANI yenye lengo la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi ambayo yana athari katika Sekta ya Kilimo na Mifugo.
Ametaja wadau watakaoshiriki ni pamoja na mashirika ya Mazingira, Kampuni za Gas, Kampuni zinazotengeneza mkaa mbadala ikiwemo STAMICO, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira pamoja na Wizara ya Nishati.
Maonesho hayo yanawakutanisha wadau wote wanaohusika katika mnyororo wa thamani wa Sekta ya Mazingira, Mifugo na Kilimo.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la REA
Mtaa wa Medeli
P. O. Box 2153,
DODOMA, TANZANIA.