Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Sasa Vijiji Vyote Mkoani Mtwara Vina Umeme
Frank A. Mugogo 38

Sasa Vijiji Vyote Mkoani Mtwara Vina Umeme

Ni furaha na nderemo kwa wakazi wa Mkoa wa Mtwara mara baada ya Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kufanikiwa kufika umeme katika Vijiji vyote 785 katika Mkoa huo.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kijiji cha Makome A ambacho ndio kijiji cha mwisho kuunganishwa na nishati ya umeme katika Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala ameipongeza REA kwa kufanikisha ndoto hiyo kutimia.
 
“Tunapinda kumpongeza sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha kwa vipindi tofauti kuhakikisha historia hii inaandikwa. Sasa tuna deni kubwa kama wananchi wa Mtwara kuhakikisha tunatumia umeme huu kujiletea maendeleo,” amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
 
Kanali Sawala pia amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya umeme kwa kuwa serikali imetumia gharama kubwa sana kufanikisha miundombinu hiyo kufika katika makazi yao.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijin (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vya mtwara kutumia kipindi hiki cha mauzo ya korosho kuhakikisha nyumba zao zinafanyiwa maandalizi ya kuingiza umeme (wiring) na kuunganisha na umeme huo REA ili malengo ya serikali yafikiwe.
 
“Gharama ya kuunganisha ni nafuu kabisa. Ni 27,000 tuu ambayo ni kodi wakati gharama zingine zote serikali imezibeba ili kuwaletea maendeleo wananchi wake. Tutumie uwepo wa umeme huu kujieletea maendeleo ya kiuchumi,” amesisitiza Balozi Kingu.
 
Awali akitoa taarifa kuhusu miradi ya REA katika mkoa huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu amesema kuwa Wakala kupitia miradi mbalimbali iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 187 imewezesha vijiji vyote 785 kupata umeme.
 
Mhandisi Olotu ameongeza pia baada ya kukamilika kupeleka umeme katika vijiji sasa wakala umeanza safari ya kupeleka umeme katika Vitongoji na kuwahamasisha wananchi kuendelea kutumia umeme huo kujiletea maendeleo yaliyokusudiwa.
 
“Mwaka 2021 vijiji 384 tuu ndio vilikuwa na umeme. Ndani ya miaka mitatu tumefanikiwa kupeleka umeme katika vijiji 401 na hivi sasa vijiji vyote 785 vina umeme. Kwenye upande wa vijiji hatuna deni. Lakini sisi kama REA hatujaishia na sasa safari ya kupeleka umeme katika vityongoji imeanza. Mkoa wa Mtwara una vitongoji hapo 3,427 na mpaka sasa vitongoji 2,200 ndio vina umeme. Tayari tunawakandarasi wanaendelea kupeleka umeme katika vitongoji, tuwaombe wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao na Wakala kwa ujumla,” amesisitiza Mhandisi Olotu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«November 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
456
Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 11.18 wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 utakaonufaisha Kaya 2,970 Mkoani Shinyanga.

Read more
78
REA Kufunga Mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia Shule ya Ruhinda

REA Kufunga Mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia Shule ya Ruhinda


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeahidi kujenga mifumo ya nishati safi ya kupikia pamoja na jiko katika shule ya Sekondari ya mchanganyiko ya Ruhinda iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.

Read more
910
111213

Report of the Controller and Auditor General on Financial and Compliance Audit for the Financial Year Ended 30 June 2023 for the Rural Energy Agency (REA)

Report of the Controller and Auditor General on Financial and Compliance Audit for the Financial Year Ended 30 June 2023 for the Rural Energy Agency (REA).

Read more
14
Call for Proposals to Supply Clean Cook Stoves for Promotions on Call Basis

Call for Proposals to Supply Clean Cook Stoves for Promotions on Call Basis

The Rural Energy Agency invites applications from qualified suppliers to submit proposals detailing the types of clean cooking solutions intending to supply clean cooking solutions across the country at subsidized rates. The proposal should also outline the actual costs and distribution expenses for providing these services in rural areas.

Read more
151617
18192021222324
2526272829301
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top