Wakala wa Nishati Vijijini (REA), chini ya Wizara ya Nishati, una jukumu la kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora na salama kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini upande wa Tanzania Bara.
Kwa kuzingatia maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia, Wakala unaandaa mpango maalum wa kuwezesha taasisi zinazoandaa chakula na kulisha watu zaidi ya 100 kwa siku kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Kupitia mpango huu, REA inakusudia kuchangia gharama za uwekezaji wa mifumo ya kisasa ya kupikia kwa njia ya ruzuku.
Wito kwa Taasisi Zote:
Ili kuandaa mpango huo, REA inaomba taasisi zote nchini kuwasilisha taarifa zao kwa kujaza fomu iliyoambatishwa na tangazo hili ambazo zitajumuisha:-
1. Jina na aina ya taasisi pamoja na eneo ilipo;
2. Idadi ya watu wanaohudumiwa kwa siku;
3. Aina ya nishati ya kupikia inayotumika kwa sasa; kiasi kinachotumika pamoja na gharama ya nishati hiyo kwa mwezi;
4. Changamoto zinazokabili taasisi katika matumizi ya nishati hiyo;
5. Mapendekezo ya mfumo au aina ya nishati safi ya kupikia inayohitajika; na
6. Mtu wa mawasiliano.
Jinsi ya Kuwasilisha Maombi:
Taasisi zinaweza kuwasilisha maombi kwa anwani iliyowekwa chini kwa kutumia njia moja kati ya zifuatazo:
• Kupitia barua pepe (clean.cooking@rea.go.tz);
• Kwa nakala ngumu (hard copy) zinazopelekwa katika ofisi za REA makao makuu au ofisi za REA za mikoa; na
• Kujaza fomu ya kielektroniki inayopatikana kwenye tovuti ya Wakala www.rea.go.tz
Muda wa Kuwasilisha Taarifa:
Ili kuwezesha Wakala kuanza kutekeleza mpango huo mapema, Taasisi husika zinatakiwa kuwasilisha taarifa zao si zaidi ya tarehe 30 Novemba 2025.
Utekelezaji wa Mpango:
Katika kutekeleza mpango huu, REA inakusudia kuchangia gharama za uwekezaji wa mifumo ya kisasa ya kupikia kwa njia ya ruzuku. Kiwango cha ruzuku kitategemea, uwezo wa taasisi husika, upatikanaji wa fedha na vipaumbele vya serikali.
Aidha, REA itaanza na taasisi zilizopo vijijini, na itapanua huduma hizo kwa maeneo mengine kwa kadri ya upatikanaji wa fedha za mpango huu kwa kuzingatia mipaka ya utekelezaji wa majukumu yake.
Taasisi zitakazoleta taarifa mapema zitafikiriwa katika awamu za mwanzo za utekelezaji wa mpango huu.
Anuani ya kutuma maombi:
Mkurugenzi Mkuu,
Wakala wa Nishati Vijijini,
Jengo la REA,
S.L.P 2153, Dodoma,
Barua pepe: clean.cooking@rea.go.tz
Tovuti: www.rea.go.tz
Kwa maelelezo zaidi wasiliana na:
1. Omari Haji Bakari
Barua Pepe: omari.bakari@rea.go.tz
Simu Namba: +255 687 013 990
2. Francis Manyama
Barua Pepe:francis.manyama@rea.go.tz
Simu Namba: +255 756 931 292
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma