Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA KAGERA
Admin.Frank Mugogo 11703

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA KAGERA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Kagera. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 11/07/2017 katika kijiji cha Rwabigaga, Kata ya Kamuli, Wilaya ya Kyerwa alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.

Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.

Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Kagera utahusisha vipengele vyote vitatu. Mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 141 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 45.43. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Aprili 2019. M/s Nakuroi Investment Company Limited ni mkandarasi atakayetekeleza Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa Kagera.

Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika Mwaka 2019 ambapo vijiji 180 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Kagera ifikapo Mwaka 2021.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

Share

Print
«December 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
252627
Zingatieni Sheria Kanuni na Taratibu- DG REA

Zingatieni Sheria Kanuni na Taratibu- DG REA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewaelekeza Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi wa umma.

Read more
2829301
234567
Kaya 19,530 Kunufaika na Majiko ya Gesi ya Ruzuku Mkoani Arusha

Kaya 19,530 Kunufaika na Majiko ya Gesi ya Ruzuku Mkoani Arusha

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Lake Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 406.7 wa kusambaza majiko ya gesi 19,530 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% katika maeneo ya vijijini ndani ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha.

Read more
8
9101112131415
16171819202122
23242526272829
303112345

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top