Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Vitongoji Vyote 64,359 Vitakuwa na Umeme Ifikapo 2030
Frank A. Mugogo 1241

Vitongoji Vyote 64,359 Vitakuwa na Umeme Ifikapo 2030

Imeelezwa kuwa hadi kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote Tanzania Bara vitakuwa vimefikishiwa nishati ya umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu Julai 05, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

"Tayari tumefikisha umeme katika vijiji vyote 12,318 Tanzania Bara sawa na asilimia 100 na sasa hivi ni zamu ya vitongoji, leo hii ninavyozungumza vitongoji 33,657 kati ya vitongoji 64,359 kote nchini vimefikishiwa umeme ambayo ni sawa na asilimia 52.3," alisema Mhandisi Olotu.

Mhandisi Olotu aliweka bayana namna ambavyo Serikali imejizatiti katika kuhakikisha umeme unafika katika kila kona ya nchi kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa usimamizi wa REA ili kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Alisema kuwa vitongoji 30,702 havijafikiwa na umeme, hata hivyo alibainisha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kupitia miradi inayotekelezwa ya kuhakikisha umeme unafika katika vitongoji hivyo.

"Katika vitongoji ambavyo havijafikiwa; vitongoji 7,736 vipo katika miradi inayoendelea kutekelezwa na vitongoji 22,966 kati ya hivi  tumetangaza zabuni kubwa ya kufikisha umeme kwenye vitongoji 9,009 hivyo tutabakiwa na vitongoji 13,957 ambavyo tunatarajia ndani ya miaka mitano navyo vitakuwa vimefikiwa kulingana na upatikanaji wa fedha," alibainisha Mha. Olotu.

Mhandisi Olotu alitoa wito kwa wananchi katika maeneo yaliyofikiwa na umeme kutumia umeme kuboresha hali ya maisha yao kwa kubuni miradi inayotumia umeme ili kujiongezea vipato vyao badala ya kutumia umeme kwa ajili tu ya mwanga wakati wa usiku.

Amewasihi kuiga mfano wa baadhi ya wananchi ambao wamevumbua fursa katika maeneo yao baada ya kufikishiwa umeme jambo ambalo limeanza kuleta manufaa katika maisha yao ya kila siku.

"Baadhi ya wanufaika tumeshuhudia namna ambavyo wamechangamkia uwepo wa umeme kwenye maeneo yao, tumekuta wanatumia umeme kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo saluni, wamefungua kumbi za kuonyesha sinema na mpira, karakana za kuchomelea na wengine wamefungua biashara ya kuuza vinywaji baridi," alisema.

Alisema kuwa katika maeneo mengi ya vijiji miji hali ya maisha imebadilika baada ya kufikishiwa umeme kwani fursa za ajira zimeongezeka kutokana na kuibuliwa kwa viwanda vidogo vidogo vingi vya kuchakata mazao.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
1213141516
REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uko katika hatua za mwisho kukamilisha mradi mkubwa wa ufungaji wa taa 214 za barabarani katika Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Tanzania (SAUT); Jijini Mwanza, hatua itakayoboresha mazingira ya usalama na kujifunzia kwa wanafunzi 13,600. Mradi huo unaoangazia barabara na maeneo ya chuo kwa urefu wa kilomita 6.42, unalenga kujenga mazingira rafiki na yenye ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao kwa urahisi wawapo chuo hapo, hususan nyakati za jioni na usiku.

Read more
1718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top