Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Watanzania Watakiwa Kuachana na Dhana Potofu Kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni Gharama
Frank A. Mugogo 545

Watanzania Watakiwa Kuachana na Dhana Potofu Kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni Gharama

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewasihi Watanzania kote nchini kuachana na dhana ya kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni gharama ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu ametoa rai hiyo Julai 04, 2025 katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam ndani ya Banda la Maonesho la Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
"Kumekuwepo na dhana kwamba kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo umeme ni gharama ikilinganishwa na kutumia kuni, dhana hii ni potofu haina ukweli kwani sasa hivi teknolojia imeboreshwa," alisisitiza Mhandisi Olotu.

Alisema kuwa kwa sasa teknolojia imeboreshwa ikilinganishwa na hapo zamani na alisisitiza kuwa hivi sasa yapo majiko ya umeme ambayo yanatumia umeme kidogo.
Alitoa wito kwa wananchi kutembelea Banda la REA ili kushuhudia teknolojia hizo zilizoboreshwa na kujionea kwa vitendo namna ambavyo majiko hayo yanafanya kazi.
"Wananchi watembelee banda la REA kujionea namna ambavyo chakula kinapikwa kwa kutumia nishati Safi ya Kupikia, ladha haibadiliki na pia muda wa kupika ni mchache ikilinganishwa na chakula kinachopikwa kwa kuni ama mkaa," alisema.

Akizungumzia kuhusiana na uhamasishaji na uwezeshwaji kwa waendelezaji wa teknojia za Nishati safi ya Kupikia, Mhandisi Olotu alisema lengo ni kuwawezesha Watanzania kutumia nishati safi kuepuka madhara ya afya ikiwemo changamoto kwenye mifumo ya upumuaji sambamba na kulinda mazingira.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya; kwa mwaka mmoja takriban watu 33,000 hupoteza maisha kutokana na matumizi ya nishati isiyo salama na kwamba REA ni miongoni mwa washika dau wa kuhakikisha idadi ya vifo vinavyosababishwa na athari ya moshi ya kuni na mkaa inapungua.

"Tunataka kuachana kabisa na matumizi ya kuni na mkaa lakini jambo hili linafanyika kwa utaratibu kwani ni ngumu kumbadilisha kila mtu mara moja; inachukua muda na ni hatua kwa baadhi ya maeneo na ndio maana kuna majiko tunasambaza yanayotumia kuni ama mkaa kwa kiwango kidogo," alisema.

Alisema kwa kuanzia REA ilianza na mpango wa kugawa majiko ya gesi ya kilo sita ambapo mitungi 3,255 na vichomeo vyake yalitolewa kwa kila Wilaya Tanzania Bara kwa bei ya ruzuku ya 50% na kwamba zoezi hili linaendelea.

"Lengo ni kumhamasisha kila mwananchi kuhama kutoka kwenye matumizi ya kuni na mkaa kuja huku kwenye nishati safi ya kupikia na kwa wale ambao tunaona inachukua muda kubadilika tumewaletea teknolojia inayotumia mkaa kidogo tukitaraji taratibu watahama," alisema.

Vilevile alibainisha kuwa REA inatekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza taasisi zinazolisha Zaidi ya watu mia kutumia nishati safi ya kupikia.

"Tunatekeleza agizo hili la Mhe. Rais tumeanza kuhamasisha na kuwezesha hizi taasisi kuhama ikiwemo Jeshi la Magereza ambapo maeneo 211 yakiwemo magereza 129, kambi za magereza 47, ofisi za mikoa za Magereza 26, nyumba za watumishi wa Magereza, vyuo, shule na hospitali zinasambaziwa nishati safi mbalimbali za kupikia," alisema.

Alizitaja nishati zilizosambazwa katika taasisi hizo kuwa ni pamoja na mifumo ya bayogesi, mifumo ya gesi ya mitungi (LPG), mifumo ya gesi asilia, mkaa unaotokana na makaa ya mawe na mashine za kutengenezea mkaa mbadala.

Aidha, alisema wakala vilevile unawajengea uwezo Maafisa wa Magereza wapatao 280 kuhusu suala zima la nishati safi ya kupikia.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma
 

Share

Print
«October 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
293012345
REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

Timu ya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na timu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tarehe 03 Oktoba, 2025 wameanza zoezi la uhamasishaji kwa Wananchi ili wajiunge na huduma ya umeme kwenye vitongoji mbalimbali vya mkoa wa Simiyu.

Read more
6789101112
13141516171819
Zaidi ya Vitongoji 2,350 Mkoani Mtwara Vyafikishiwa Umeme

Zaidi ya Vitongoji 2,350 Mkoani Mtwara Vyafikishiwa Umeme

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefikisha umeme katika vitongoji 2,354 kati ya vitongoji 3,421 Mkoani Mtwara huku ukiendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vilivyosalia mkoani humo.

Read more
20
Newala Waipa Kongole REA Mradi wa Kusambaza Umeme Vitongojini

Newala Waipa Kongole REA Mradi wa Kusambaza Umeme Vitongojini

Wakazi wa vitongoji vya Chihanga, Mpilipili, Mkwedu na Majengo Wilayani Newala Mkoani Mtwara wameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufikisha umeme katika vitongoji hivyo.

Read more
2122
Tangazo Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100 Kuhusu Uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Tangazo Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100 Kuhusu Uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), chini ya Wizara ya Nishati, una jukumu la kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora na salama kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini upande wa Tanzania Bara.

Read more
23242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top