Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi
Frank A. Mugogo 17

Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amuopengeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi kubwa ya kufikisha umeme vijijini hali iliyobadili maisha ya wananchi vijijini.
 
Mhe. Dendego ametoa pongezi hizo leo Aprili 11, mkoani Singida wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Mwaka kati ya Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati (EDPG) pamoja na REA uliolenga kupitia bajeti na mpango kazi wa Wakala huo kwa mwaka 2025/26.
 
“Nishati ya umeme ni nguzo kubwa kwa maendeleo ya Taifa lolote na watu wake. Nishati ya umeme vijijini ni msingi mkuu wa kuimarisha maendeleo ya haraka katika vijijini vyetu. Sote tumeshuhudia matokeo makubwa kwenye ukuaji wa uchumi, kuboresha maisha ya jamii zetu pamoja na kuchagiza utoaji wa huduma za kijamii.
 
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imelipa swala la umeme vijijini kipaumbele cha kipekee na kuliweka katika mipango yake. Sekta ya Nishati, hasa nishati ya umeme vijijini kazi kubwa imefanyika. Tuwapongeze sana,” amesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida.
 
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatib Kazungu amewashukuru Wabia hao wa Maendeleo na kusema kuwa wamekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya nishati nchini huku akiwahakikishikia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha lengo la kuwafikishia nishati bora kwa bei nafuu wananchi wote linafikiwa.
 
Awali akizungumza, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meje Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu amesema kuwa, Tanzania imepiga hatua kubwa katika usambazaji wa umeme vijijini na mafanikio hayo yametokana na dhamira ya Serikali pamoja na mchango wa Wabia wa Maendeleo na kuahidi kuwa, REB itaendelea kuisimamia Mejimenti ya REA kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inafanikiwa kwa wakati na katika ubora uliokusudiwa.
 
Naye Mwenyekiti wa Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati (EDPG), Kjetil Schie ameipongeza REA kwa kazi kubwa ya kusambaza umeme vijijini na kuahidi kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta ya nishati.
 
“Tumeona ni kwa namna gani umeme unavyoweza kuboresha huduma za kijamii kama huduma za afya, upatikanaji wa maji na pia katika sekta ya elimu. Tulianza kushirikiana tukiwa na lengo la kutamani kuona kila Mtanzania akipata nishati ya umeme, na siku zinavyoenda tunaona lengo hilo linaenda kutumia. Tunapata matumaini sana na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Serikali kufikia lengo hilo,” amesema Schie.
 
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu amewashukuru na Wabia hao wa Maendeleo ambao ni Umoja wa Ulaya (EU), Benki ya Dunia, Serikali ya Norway, Serikali ya Sweden, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), Benki ya Maendeleo ya Afrika na kuahidi kuwa REA itaendelea kutekeleza miradi kwa wakati na ubora uliopangwa ili dhamira ya Serikali pamoja na Wabia hao wa Maendeleo ya kuhakikisha kila mwananchi anapata nishati ya umeme inafikiwa.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«April 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
311234
CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

The Rural Energy Agency issue the Second Call for applications from qualified suppliers to Supply and install Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions through on-call basis.

Read more
56
789
Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Please find the attached Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24:

Read more
10111213
14
Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amuopengeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi kubwa ya kufikisha umeme vijijini hali iliyobadili maisha ya wananchi vijijini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top