Friday, June 23, 2017 Admin.Frank Mugogo 9539 News ZIARA YA VIONGOZI WA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) KATIKA WILAYA YA KILOLO Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga aliongoza ujumbe wa viongozi wa Wakala ziara ya siku moja iliyofanyika tarehe 17/06/2017 katika Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa.Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kutathmini matokeo chanya yaliyotokana na utekelezwaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini katika wilaya ya Kilolo ambapo wilaya hiyo ni mojawapo ya wilaya zilizopatiwa miradi ya awali ya Wakala ambayo ilitekelezwa katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2008 hadi Mwaka 2010.Wilaya ya Kilolo, ambayo ina jumla ya wateja waliounganishiwa umeme 2,961, imeendelea kunufaika na awamu nyingine za miradi ya Wakala. Miongoni mwa wateja hao waliounganishwa ni shule za msingi 10, shule za sekondari 10, zahanati 9 na pampu ya maji. Pia mashine za kusaga na kukoboa nafaka, mashine za kuranda mbao na kuchomelea vyuma zimeunganishwa na huduma za umeme.Miradi ya kusambaza umeme vijijini katika Wilaya ya Kilolo imechochea shughuli za uzalishaji mali na biashara katika nyanja za kilimo na ufugaji ambapo kuna mashamba makubwa kama ya Ndoto Farm, Makota Farm na Bill Clinton Foundation yanaendeshwa kwa kutumia huduma za umeme. Pia viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao ya kilimo vimeunganishwa na huduma ya umeme.Imetolewa na:Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2Barabara ya Sam NujomaS. L. P 7990Dar es Salaam, TanzaniaBarua Pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003Nukushi: +255 22 2412007 Tags News Share Print Switch article MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KITAIFA YALIYOFANYIKA KIJIJI CHA , BUTIAMA, MKOA WA MARA Previous Article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MANYARA Next Article