Thursday, April 13, 2017 Admin.Frank Mugogo 10292 News UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA DODOMA Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Dodoma. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 16/03/2017 katika kijiji cha Kigwe Wilaya ya Bahi alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Dodoma utahusisha vipengele vyote vitatu. Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 182 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 75. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2019.Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika mwaka 2019 ambapo vijiji 166 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya mkoa wa Dodoma ifikapo Mwaka 2021.Imetolewa na:Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2Barabara ya Sam NujomaS. L. P 7990Dar es Salaam, TanzaniaBarua Pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003Nukushi: +255 22 2412007 Tags News Share Print Switch article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA PWANI Previous Article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MARA Next Article