Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA PWANI
Admin.Frank Mugogo 13158

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA PWANI

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Pwani. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 13/03/2017 katika kijiji cha Msufini Wilaya ya Kibaha alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.

Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.

Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Pwani utahusisha vipengele vyote vitatu. Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 204 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 30.2. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi, 2019.

Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika Mwaka 2019 ambapo vijiji 127 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya mkoa wa Pwani ifikapo Mwaka 2021.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

Share

Print
«February 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
27
Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika - Misheni 300 ni kichocheo cha maendeleo ya nchi za Afrika na kichocheo cha utekelezaji wa Sera yake ya Taifa ya Nishati inayolenga kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi.

Read more
2829303112
3456789
1011121314
REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na kampuni ya Oryx Gas Tanzania, tarehe 12 Februari, 2025 imeanza rasmi kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa wakazi wa mkoa wa Songwe na kwa kuanzia Wananchi wa wilaya ya Mbozi wameanza kununua mitungi hiyo kwa nusu bei.

Read more
1516
17181920212223
242526272812
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top