Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
NORWAY YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 200 KWA AJILI YA UMEME VIJIJINI
Host 12005

NORWAY YAISAIDIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 200 KWA AJILI YA UMEME VIJIJINI

Serikali ya Tanzania imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada wa Krona milioni 700, sawa na shilingi bilioni 200 za Tanzania, kutoka Serikali ya Norway, kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisaini mkataba wenye makubaliano hayo, Aprili 9, 2013 Mjini Oslo Norway akiiwakilisha Serikali ya Tanzania, ambapo Serikali ya Norway iliwakilishwa na Waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Heikki Holmas.

Zoezi la kusaini mkataba huo lilifanyika mwishoni mwa Mkutano ambao Waziri Muhongo alishiriki uliobeba dhima isemayo ‘Nishati na Maendeleo Kuanzia 2015’. Malengo mahsusi ya mkutano yalikuwa ni kufanya majumuisho ya majadiliano mbalimbali kuhusu nishati ambayo yamekuwa yakifanyika ulimwenguni kote na katika mitandao, na pia kutoa mapendekezo kuhusu nafasi ya nishati katika maendeleo kuanzia mwaka 2015.

Akizungumzia msaada huo, Prof. Muhongo alisema “sasa tunao uhakika wa kumaliza miradi ya umeme kwenye Wilaya mpya 13, zoezi litakalogharimu takribani shilingi bilioni 70 za kitanzania, na pia kukamilisha miradi mingine ya umeme vijijini”.

Kwa upande wake, Waziri Holmas alisema “kuwapatia watu waishio vijijini huduma ya umeme ni sawa na kuwapatia Watanzania wengi uwezekano wa kuondokana na matumizi ya nishati zenye uharibifu kama mafuta ya taa na dizeli.” Alifafanua kuwa msaada huo unalenga kuleta usawa kwa vitendo, ambao utainua hali ya maisha haraka na kuleta njia mbadala za kujipatia kipato kwa wananchi wa vijijini.

Alisema, zaidi ya asilimia 90 ya msaada uliotolewa itatumika kuweka umeme kwa kuongeza miundombinu ya usambazaji wa umeme, ambapo kwa mujibu wake ndiyo namna nzuri zaidi ya kuyafikia maeneo ya vijijini kwa huduma husika, kulingana na uzoefu.

Profesa Muhongo alisema Tanzania imedhamiria kuongeza huduma ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa Watanzania kutoka asilimia 18.4 hadi 30 kwa ngazi ya taifa, na kutoka asilimia 6.5 hadi 15 kwa maeneo ya vijijini.

Baada ya Mkutano na makubaliano hayo, Waziri Muhongo ameendelea na safari yake katika Mji wa Brussels, Ujerumani akiendelea na zoezi la kutafuta fedha za miradi mbalimbali ya umeme.

Imeandaliwa na:

Fadhili P. Kilewo
Mkuu wa Idara ya Habari
Wizara ya Nishati na Madini
754/33, Samora Avenue
S. L. P. 2000
Dar es Salaam, Tanzania
info@mem.go.tz
www.mem.go.tz

Share

Print
«September 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
26
REA yamtaka mwendelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Maguta mkoani Iringa kuongeza kasi

REA yamtaka mwendelezaji wa mradi wa kufua umeme wa Maguta mkoani Iringa kuongeza kasi

Serikali imemtaka Mwendelezaji wa Mradi wa kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji wa Maguta  uliopo katika Kijiji cha Masisiwe Wilayani Kilolo Mkoani Iringa kuukamilisha kwa wakati.

Read more
27
Wananchi waaswa kutunza mazingira

Wananchi waaswa kutunza mazingira

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewaasa wananchi kutunza mazingira na kulinda miundombinu pamoja na vyanzo vya maji ili kuendelea kupata huduma ya umeme pamoja na kuwa na miradi endelevu ya kufua umeme.

Read more
282930311
2345678
9101112
EXTENDED DEADLINE FOR INVITATION FOR PROPOSALS - Supply of Starter Packs of LPG for Prison Staffs in Areas of Rural Mainland Tanzania

EXTENDED DEADLINE FOR INVITATION FOR PROPOSALS - Supply of Starter Packs of LPG for Prison Staffs in Areas of Rural Mainland Tanzania

The Government of Tanzania through the Rural Energy Agency (REA) in collaboration with Tanzania Prisons Services (TPS) in response to attainment of sustainable development goals, has opened a   financing   window to support distribution of 15,920 units of 15kg LPG Starter Packs to earmarked Staffs in all Tanzania Prisons. This is part of the Clean Cooking Packages that the parties have agreed to cooperate inorder to enable these institutions to stop using environmentally and healthily harmful cooking solutions.

Read more
131415
16171819202122
23242526272829
30123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
PSSSF Building, 7th Floor
Makole Road
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top