Bodi ya Nishati Vijijini Yatembelea Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere
Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imefanya ziara ya siku moja katika Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere uliopo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao ukikamilika utawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.
Katika ziara hiyo iliyofanyika Oktoba 03, 2020 Bodi ilijumuika pamoja na ujumbe wa Wizara ya Nishati ambao uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Mhandisi Leonard Masanja.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhandisi Masanja alisema kuwa mahitaji ya umeme yataongezeka kutokana na utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini ambayo inaibua fursa za uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo na vya kati pamoja na shughuli nyingine za uzalishaji mali.
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7
S. L. P 2153
Dodoma, Tanzania
Barua pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507