Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Wananchi Kahama Wamshukuru Rais Samia Kuwafikishia Umeme wa REA
Mohamed Saif 199

Wananchi Kahama Wamshukuru Rais Samia Kuwafikishia Umeme wa REA

Shughuli za kiuchumi na kijamii zimeimarika

Wananchi Kata za Wendele na Mwendakulima Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kubadilisha maisha yao kupitia mradi wa umeme uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Wametoa shukrani hizo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba kwa nyakati tofauti Januari 10, 2026 wakati wa hafla ya kuwasha umeme kwenye kitongoji cha Majengo Kata ya Wendele na Kitongoji cha Chapulwa Kata ya Mwendakulima.

"Ni neema kubwa kupata umeme, tunaishukuru Serikali kwa kutufikishia umeme, maisha yetu yanabadilika," alisema Mariam Manyesha Mkazi wa Kitongoji cha Majengo.

Mara baada ya kuwasha umeme, Naibu Waziri Mhe. Salome alizungumza na wananchi na kuwaeleza namna ambavyo Serikali imejipanga kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi - CCM (2025-2030).

Mhe. Salome alibainisha kuwa Rais Samia ameelekeza ndani ya mwaka huu kaya 1,700,000 nchini wawe wameunganishwa na huduma ya umeme na kwamba tayari utekelezaji wa maelekezo hayo unaendelea. 

"Niwahakikishie tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais, umeme ni kichocheo cha uchumi tumeshuhudia mabadiliko makubwa kwenye maeneo yaliyofikishiwa umeme na kipaumbele chetu ni kuwasha umeme," amesema Mhe. Salome.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mha. Jones Olotu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, alieleza namna ambavyo REA imejipanga kufikisha umeme kwenye vitongoji vyote nchini.

Alisema REA inaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme vitongojini na kwamba hivi karibuni itasainiwa mikataba ya kusambaza umeme katika vitongoji 9009 kote nchini.

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top