Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kaya 19,530 Kunufaika na Majiko ya Gesi ya Ruzuku Mkoani Arusha
Frank A. Mugogo 80

Kaya 19,530 Kunufaika na Majiko ya Gesi ya Ruzuku Mkoani Arusha

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Lake Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 406.7 wa kusambaza majiko ya gesi 19,530 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% katika maeneo ya vijijini ndani ya Wilaya ya Arusha, Karatu, Longido, Meru, Monduli na Ngorongoro Mkoani Arusha.
 
Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amebainisha hayo Desemba 6, 2024 Mkoani Arusha wakati wa kumtambulisha mtoa huduma huyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

"Tumeanza utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao unasisitiza miaka 10 kutoka sasa 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, na hili linaweza kufikiwa kupitia mbinu na mikakati mbalimbali ikiwemo hii ya usambazaji wa majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku," alisema Mhandisi Yesaya. 

Alifafanua kuwa REA imeandaa programu mbalimbali ili kufanikisha azma hiyo ya Serikali ambayo imeasisiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulinda afya za wananchi wake sambamba na kuhifadhi mazingira kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za Nishati Safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti ambapo alibainisha kuwa takribani hekta 400,000 hukatwa kila mwaka.

"Mradi huu unakwenda kusaidia kuondokana na athari za kiafya, pia utasaidia kuepuka vitendo vya kikatili, kulinda vyanzo vya maji na kutunza Mazingira na pia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi," alifafanua Mhandisi Yesaya.
 
Aidha, alisema kuwa mradi huo vilevile ni nyenzo muhimu ya kupunguza umaskini miongoni mwa jamii za maeneo ya vijijini kwani utatoa fursa kwa akina mama kujikita katika shughuli za uzalishaji mali pindi wanapotumia mitungi ya gesi kama njia mbadala ya kupikia sababu inaokoa muda ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Missaile Musa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango huo ambao amesema unakwenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo wa kumudu gharama ya manunuzi ya majiko hayo ya gesi.

"Tunashukuru kwa mawazo haya ya Mhe. Rais na kwa kazi inayofanywa na REA. Ninaamini kwa ruzuku hii iliyowekwa na Serikali, Watanzania walio wengi wataweza kumudu gharama na hii itafanikisha lengo la 80% ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034," alisema.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Lake Gas, Kanda ya Kaskazini, Ismail Juma alithibitisha kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha wanufaika wa majiko hayo wanafikiwa kikamilifu na alitoa wito kwa wananchi mkoani humo kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali kupitia REA.

Alitoa rai kwa wananchi kutumiza masharti ya kupata majiko hayo ya ruzuku ikiwa ni pamoja na kuwa na kitambulisho cha Taifa cha NIDA ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa kila mwananchi.

Wakala wa Nishati Vijijini unatekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao ulizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei mwaka huu.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top