Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Majiko ya Gesi 19,530 Kusambazwa kwa Bei ya Ruzuku Mkoani Kilimanjaro
Frank A. Mugogo 17

Majiko ya Gesi 19,530 Kusambazwa kwa Bei ya Ruzuku Mkoani Kilimanjaro

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatarajia kusambaza jumla ya majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita 19,530 yanayotolewa kwa bei ya ruzuku ya 50% Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034. 

Hayo yameelezwa Desemba 6, 2024 na Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya Mkoani Kilimanjaro wakati wa kutambulisha mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku sambamba na kumtambulisha msambazaji ambaye ni Kampuni ya Lake Gas katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. 

"Tumeanza utekelezaji wa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku tupo hapa kutambulisha rasmi mradi huu unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 407 kwa mkoa huu na pia  kumtambulisha msambazaji katika mkoa huu ambaye ni Kampuni ya Lake Gas," amesema Mhandisi Yesaya. 

Mhandisi Yesaya amesema REA imejipanga kutekeleza azma ya Serikali inayoongozwa na Rais. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha ifikapo mwaka 2034; 80% ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia. 

Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Nzowa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, aliipongeza REA kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza dhamira na ajenda kuu ya Rais. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.
 
"Tunashuhudia REA inatekeleza kwa vitendo dhamira ya Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi kupikia na wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa ili kulinda kuhifadhi mazingira na pia kulinda afya," amesema. 

Ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuchangamkia fursa hiyo iliyotolewa na Serikali kupitia REA hasa ikizingatiwa kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia yanaokoa gharama na muda ambao mwananchi anaweza kutumia kufanya shughuli nyingine za kiuchumi lakini pia ni rafiki wa mazingira na afya kwa mtumiaji.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi kwa ujumla, Mhandisi Yesaya amesema kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025, jumla ya majiko ya gesi 452,445 ya kilo sita yenye thamani ya shilingi bilioni 10 yatasambazwa kote nchini kwa bei ya ruzuku ya asimilia 50.
 
Mhandisi Yesaya ameeleza kuwa mbali ya mradi huo wa usambazaji wa majiko ya gesi; REA vilevile inaandaa mradi wa kusambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambapo alisema jumla ya majiko 200,000 yatasambazwa kwa bei ya ruzuku ya 75% hadi 85% kwa maeneo ya vijijini kote nchini. 

Amesema lengo ni kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa kulingana na hali yake ya kiuchumi ili kufikia lengo kuu la mkakati la kufikisha 80% ya watanzania watakaotumia nishati safi na iloyo bora ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«December 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
252627
Zingatieni Sheria Kanuni na Taratibu- DG REA

Zingatieni Sheria Kanuni na Taratibu- DG REA

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewaelekeza Watumishi wa Wakala wa Nishati Vijijini kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi wa umma.

Read more
2829301
2345678
91011
Arusha Wamshukuru Rais Samia

Arusha Wamshukuru Rais Samia

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha wamemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi wa kusambaza majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku ya 50% katika halmashauri hiyo.

Read more
12131415
16171819202122
23242526272829
303112345

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top