Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kituo cha Kupoza Umeme Mtera Kuboresha Upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma
Mohamed Saif 288

Kituo cha Kupoza Umeme Mtera Kuboresha Upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Mtera (2x10MVA, 220/33kV) ambacho kitaongeza ubora wa umeme, kupunguza changamoto ya umeme mdogo na kuboresha huduma za kijamii, afya, elimu, maji na mawasiliano.

Akizungumza katika hafla hiyo Januari 16, 2026 mkoani Iringa, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema upanuzi wa kituo cha Mtera ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha nishati ya umeme inapatikana kwa uhakika na kwa gharama nafuu kwa wananchi katika maeneo ya vijijini. 

Halikadhalika ameongeza kuwa, mradi huo utawanufaisha wananchi wa wilaya za Mpwapwa na Kongwa mkoani Dodoma, pamoja na wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, kwa kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii.

"Umeme upo wa kutosha, niwaombe wananchi wajitokeze kuunganishiwa umeme ili waweze kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na upatikanaji wa nishati ya uhakika,” amesema Mhe. Ndejembi

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema REA imeleta mapinduzi makubwa katika kufikisha umeme vijijini, akibainisha kuwa mwaka 2014 ni asilimia 7 pekee ya wananchi wa vijijini waliokuwa na umeme, huku mwaka 2026 kiwango hicho kimefikia asilimia 78.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Simon Lusengekile, amepongeza mikakati ya Serikali kupitia REA katika kuwahudumia wananchi kupitia miradi ya nishati, huku akiwataka wananchi kulinda miundombinu ya umeme ili iweze kudumu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Aidha, Mwakilishi wa Wabia  wa Maendeleo ambao ni Norway na Sweden, Stephen Mwakifwamba, ambao wamechangia gharama za ujenzi wa Kituo  cha Kupoza Umeme cha Mtera amesema kuwa wamefurahishwa na mafanikio ya utekeleza wa mradi ambao umeanza kuwanufaisha wananchi wa mikoa ya Iringa na Dodoma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Balozi Jacob Kingu, ameipongeza Menejimenti na watendaji wa REA kwa kukamilisha mradi huo kwa mafanikio, akisisitiza kuwa wakala una mchango mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya nishati nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, amebainisha kuwa Kituo cha Mtera kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9.2 na Serikali ya Tanzania kupitia REA kwa ushirikiano na Serikali za Sweden na Norway.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Iringa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, amesema mradi huo utawanufaisha kwa kiasi kikubwa wananchi wa mikoa hiyo, huku akiipongeza REA kwa kazi kubwa ya kufikisha umeme vijijini.

Amesema licha ya kuwepo kwa umeme wa kutosha, matumizi ya sayansi na teknolojia ni muhimu katika kuhakikisha umeme haukatiki mara kwa mara, akiongeza kuwa miradi kama hiyo inaonesha mchango wa sayansi katika kupunguza changamoto za umeme.

Aidha, amewahimiza wananchi wa wilaya za Kongwa na Mpwapwa kutumia fursa ya umeme wa uhakika kuongeza uzalishaji wa viwandani na kuboresha uchumi wa Mkoa wa Dodoma kwa ujumla.

 

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top