Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Serikali Kupitia REA Kuzindua Miradi Mikubwa Ya Kimkakati
Mohamed Saif 399

Serikali Kupitia REA Kuzindua Miradi Mikubwa Ya Kimkakati

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kuzindua Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Mtera na Kusaini Mikataba ya kutekeleza mradi kabambe wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 9,009 katika Mikoa yote Tanzania Bara.

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy amesema hayo Jijini Dodoma Januari 15, 2026 katika mkutano maalum na wanahabari  alipokuwa akitambulisha matukio hayo mawili yatakayoshuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ambaye atakuwa mgeni rasmi.

“Tarehe 16 Januari, 2026 Kituo cha Kupoza Umeme cha Mtera kitazinduliwa rasmi na tarehe 17 Januari, 2026 tutasaini mikataba 30 yenye thamani ya shilingi Trilioni 1.2 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa kusambaza umeme katika vitongoji zaidi ya 9,000,” amefafanua Mha. Saidy

Amebainisha kuwa Kituo cha Mtera kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 9.2 na Serikali ya Tanzania kupitia REA kwa ushirikiano na Serikali za Sweden na Norway.

Aidha, Mhandisi Saidy amesema REA itasaini mikataba 30 na Wakandarasi 21 wazawa na wakandarasi 9 kutoka nje ya nchi lakini wamesajiliwa nchini kwa ajili ya kutekeleza mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu ndani ya Mikoa yote Tanzania Bara.

Amewataka wananchi kuchangamkia fursa zitakazopatikana wakati wote wa utekelezaji wake ikiwemo ajira, biashara na huduma mbalimbali zitakazohitajika na pia kuhakikisha wanachangamkia kutumia umeme kuzalisha mali na kuboresha huduma za kijamii.

“Tunatekeleza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan; mradi huu unakwenda kufungua nchi kiuchumi ni wa kipekee na mradi mkubwa kuwahi kutekelezwa na REA kwa viwango vya gharama na idadi ya vitongoji vitakavyofikiwa,” amesema Mha. Saidy.

Share

Print
«August 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
1011121314
REA Yaeleza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Kwenye Tamasha La Kizimkazi Mwaka 2026

REA Yaeleza Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Kwenye Tamasha La Kizimkazi Mwaka 2026

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefanikiwa kusambaza takribani mitungi laki saba ya gesi ya kupikia (LPG) nchini kote, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kasi wa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Read more
1516
17181920212223
24252627282930
31123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top