Saturday, July 20, 2019 Admin.Frank Mugogo 6378 News, Announcements Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Kufanikisha Azma ya Serikali Kujenga Uchumi wa Viwanda Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo amesema miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa katika wilaya na mikoa yote Tanzania Bara itafanikisha azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo Mwaka 2025.Wakili Kalolo alisema hayo wakati wa ziara ya Bodi hiyo katika banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yaliyofanyika kuanzia tarehe 28/06/2018 hadi 13/07/2019 jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, Bodi ya Nishati Vijijini itasimamia utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini ili kuhakikisha kuwa lengo la Serikali linafikiwa.Aidha, Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Nishati Vijijini alihimiza kuwa wananchi waanzishe viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao ya mimea, mifugo na uvuvi pamoja na viwanda vingine katika maeneo ambayo tayari yamepelekewa huduma ya umeme na kusema kuwa, huduma ya umeme itafikishwa katika kila Kijiji Tanzania Bara ifikapo Mwaka 2021.Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Jengo la LAPF, Ghorofa ya 7S. L. P 2153Dodoma, TanzaniaBarua pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 262323504, +255 262323506, +255 262323507 Share Print Switch article Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Merdard Kalemani Aagiza Kuharakisha Utekelezaji wa Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Previous Article Bodi ya Nishati Vijijini Yapongeza Uzalishaji wa Vifaa vya Miradi ya Umeme Next Article