Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika
Frank A. Mugogo 416

Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika - Misheni 300 ni kichocheo cha maendeleo ya nchi za Afrika na kichocheo cha utekelezaji wa Sera yake ya Taifa ya Nishati inayolenga kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi. 

Dkt. Biteko amesema hayo leo Januari 27, 2025 wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia leo Januari 27 - 28, 2025 ambapo majadiliano yamehusisha ngazi ya Mawaziri na Wataalam wengine kutoka Serikalini na wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Mkutano na majadiliano hayo utafuatiwa na mkutano wa viongozi wakuu wa nchi za Afrika, wawakilishi na viongozi wengine na utafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Biteko amesema pamoja na maendeleo ya nishati yaliyofikiwa, bado nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati mbadala ikiwa na matarajio ya kukuza shughuli za kiuchumi hususan katika sekta za viwanda na madini jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati zaidi katika sekta ya nishati.  

Kwa bara la Afrika pia, pamoja na mafanikio  makubwa ya kuzalisha umeme barani hapa, takriban Waafrika milioni 571 bado hawana huduma ya umeme hivyo, mkutano huu umeitishwa rasmi kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo.  

"Sera hiyo pia inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati na kuongeza mchango wa nishati mbadala katika mchanganyiko wa uzalishaji ili kuimarisha upatikanaji, uhakika na usalama wa nishati", amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa, Rais  Samia amekuwa mstari wa mbele katika kukuza upatikanaji wa suluhisho la nishati safi ya kupikia barani Afrika, jitihada ambazo zimeungwa mkono na mkakati wa kitaifa na kujumuishwa katika Azimio litakalotiwa saini katika mkutano huo, huku wakitoa wito wa ahadi na ushirikiano zaidi katika kuboresha upatikanaji wa suluhisho la nishati safi ya kupikia barani mwetu.  

Aidha, amesisitiza kuwa ifikapo mwishoni wa mwaka 2025, uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme utaongezeka hadi kufikia megawati 4,000, nishati inayotoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo nishati jadidifu kwa lengo la kunufaisha wakazi wa vijijini na mijini, huku miundombinu ya umeme ikifikia vijiji vyote 12,318 nchini.  

Pia, Tanzania inaimarisha muunganiko wa Afrika kwa kuwa na miundombinu ya umeme inayounganisha nchi za Kenya, Burundi, Rwanda, na Uganda, huku miundombinu ya kuunganisha  na Zambia ikiwa inaendelea.  

Ametaja mambo mengine yatakayofanyika katika mkutano huo kuwa ni kushirikishana uzoefu; kupata ahadi muhimu za kisiasa; kutumia ushirikiano ili kufungua uwekezaji wa sekta binafsi; kuanzisha ushirikiano wa kufadhili miundombinu ya nishati; na kukubaliana mfumo wa ufuatiliaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha Kiashiria cha Ufuatiliaji wa Maazimio ili kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwenye mkutano huo.  

Ametoa rai kwa viongozi walioshiriki mkutano huo kutumia fursa hiyo kuhitimisha Maazimio yanayoendana na matarajio ya bara la Afrika ya nishati na kuimarisha ushirikiano unaohitajika katika kuyatekeleza.

"Ni matarajio yangu kwamba, mamlaka zinazohusika za nishati katika kila nchi ya majaribio zitajitahidi kuhakikisha maazimio ya nishati yanafanikishwa kupitia malengo na mipango ya hatua zinazolenga kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme, matumizi ya nishati safi ya kupikia, nishati mbadala na mchango wa mtaji wa sekta binafsi katika kufanikisha upatikanaji wa nishati", amemalizia Dkt. Biteko.  
Kwa upande wake, Rais wa Benki ya Dunia (WB), Bw. Ajay Banga amesema kuwa bara la Afrika linaweza kubadilisha sura ya Afrika kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi Afrika ifikapo 2030

Rais huyo wa WB, amepongeza kwa dhati juhudi za Rais Samia kuwa kinara wa maendeleo ya nishati, Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Amesema hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana gizani hivyo, njia ya kuleta maendeleo na ustawi wa watu ni kuwaangaza maisha yao kwa kupitia sekta ya Nishati.

Naye, Rais wa Benki ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinumwi Adesina ameipongeza nchi ya Tanzania kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kufanya vizuri katika uwekezaji wa miundombinu ya umeme kwa kuwafikishia nishati ya umeme wananchi katika vijijini vyote 12,318.

Amesema kuwa ili kufanikisha mpango wa maendeleo ya watu ni muhimu kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.

" Majadiliano ya aina hii yanafungua milango kuelekea maendeleo na ustawi wa watu wa Afrika" na kuongeza kuwa ili kufikiwa kwa malengo hayo taasisi husika zinahitaji kuzungumza na kuhakikisha upatikanaji wa fedha"

Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Nishati, Viongozi wa Taasisi za Kimataifa za Kifedha, Wataalam na Wadau wa Mashirika ya Kiraia ambao watapata fursa ya kujadili na kukubaliana malengo, vipaumbele vya sera, suluhisho, na ahadi za jinsi ya kutekeleza Mpango wa Mission 300.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
293012345
REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

Timu ya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na timu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tarehe 03 Oktoba, 2025 wameanza zoezi la uhamasishaji kwa Wananchi ili wajiunge na huduma ya umeme kwenye vitongoji mbalimbali vya mkoa wa Simiyu.

Read more
6789101112
13141516171819
Zaidi ya Vitongoji 2,350 Mkoani Mtwara Vyafikishiwa Umeme

Zaidi ya Vitongoji 2,350 Mkoani Mtwara Vyafikishiwa Umeme

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umefikisha umeme katika vitongoji 2,354 kati ya vitongoji 3,421 Mkoani Mtwara huku ukiendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vilivyosalia mkoani humo.

Read more
20
Newala Waipa Kongole REA Mradi wa Kusambaza Umeme Vitongojini

Newala Waipa Kongole REA Mradi wa Kusambaza Umeme Vitongojini

Wakazi wa vitongoji vya Chihanga, Mpilipili, Mkwedu na Majengo Wilayani Newala Mkoani Mtwara wameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kufikisha umeme katika vitongoji hivyo.

Read more
2122
Tangazo Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100 Kuhusu Uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Tangazo Kwa Taasisi Zinazohudumia Watu Zaidi ya 100 Kuhusu Uhamasishaji wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), chini ya Wizara ya Nishati, una jukumu la kuhamasisha na kuwezesha upatikanaji wa nishati bora na salama kwa wananchi walioko maeneo ya vijijini upande wa Tanzania Bara.

Read more
23242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top